Member of EVRS

Thursday, 9 December 2010

Unaelewa Nini Kuhusu Uhuru wa Tanganyika

Leo, watanganyika (hata kama huupendi huu ukweli), wamesheherekea miaka 49 tangu wapate uhuru wao kutoka kwa mkoloni (Uingereza). 
  
Asilimia kubwa ya watu wanaofuatilia uhuru huu, wanaukandia na kuubomoa, na kuona hauna maana kubwa kwa hali halisi ya kiuongozi tulionao na watendaji wengine. 
  
Mkulima wa kijijini, ndio kwanza haelewi hata maana ya uhuru wenyewe.
Kwa wale wanaokenua meno na kushangilia siku ya uhuru, wanapaswa kujiuliza kwa nini watnganyika wengine hawaelewi kabisa maana ya siku na uhuru wenyewe.  
  
Nina hakika uhuru wenye maana kwa wananchi, kila mtu huwa anaguswa na siku hii, lakini kwa watanganyika, naona huwa wanajua kwa kuwa siku hiyo hawatakiwi kwenda kazini, na pia kushuhudia gwaride la kijeshi, baada ya hapo hawajui chochote.

Mchambuzi Fadhy Mtanga, kaeleza mtazamo wake kuhusu uhuru wa Tanganyika, soma makala yake hapa

4 comments:

Crissant said...

Thanks for your words, my friend!
I wish you all the best!
Have a sweet Christmas and Great 2011!
See you!

Fadhy Mtanga said...

ahsante sana kaka Chib kwa kupita kibarazani kwangu na kuacha maoni. pia nakushukuru sana kwa kuweka kiungo cha makala yangu.

SIMON KITURURU said...

Uhuruuu!

Ngojea tu nikae kimya!

emu-three said...

Jamaaa kasema kuwa sio MTANGANYIKA, NIMDANGANYIKA...Kwanini kasema hivyo eti kwasababu tulidanganywa kuwa tumepata uhuru kumbe ni `ushuru'!
Leo miaka 49, umeme hakuna, sisi wa Gongo la mbali uhuru mchana hatukuuona, maana uhuru na sherehe mabalimbali twaziona kwenye runinga, utazionaje wakati hakuna umeme...fikiria miaka 49, bado tatizo la umeme ni kitendawili..! Mtu mzima, mwenye busara, hajajua lini atalitatua hili, mpaka BWANA MKUBWA MFADHILI...Ambaye leo twasherehekea kutupa uhuru..hajatupa uhuru katupa `ushuru' ili kila kukicha tukamlipe...kwa vipi? Changanya bongo lako!