Member of EVRS

Wednesday, 8 December 2010

Mstaafu ateuliwa kushika Nyadhifa ya Mstaafu

Rais Jakaya Kikwete amemteua Jaji Mstaafu Salome Suzette Kaganda kuwa Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma. Uteuzi huo ulianza tangu tarehe 4 Desemba 2010. 
  
Jaji mstaafu Salome amechukua nafasi ya jaji mstaafu Stephen Ihema ambaye amemaliza muda wake.  
Taarifa hizi zimetolewa na Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu.
   
Tukumbuke pia kuwa tume ya uchaguzi inaongozwa na Jaji Mstaafu Lewis Makame.  
  
Sielewi vizuri hii dhana ya kuchagua wastaafu kuwarithi wastaafu.
Ningependa kusikia watyu wenye uwezo ambao hawajastaafu wakishikilia nyadhifa hizo na watu wengine wanaochipukia wakibana nafasi za wenzao wanaopanda nyadhifa, na sio kila siku wastaafu ndio wanashika hatamu.
Suala hili lingeenda pia na kwa wakuu wa vyuo vikuu, weneyviti wa bodi mbalimbali kwani wengine wako hoi sana kwa uzee na sioni sababu ya wao kuendelea kukamata nyadhifa hizo.

5 comments:

Fadhy Mtanga said...

nami siielewi kabisa hii tabia ya wastaafu kushika madaraka haya....hali hii inawafungia milango watu chungu mbovu wenye uwezo.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sijui kama uko sahihi au kwa sababu wewe hujakaribia kustaafu ili uwe frustrated?

sasa akichagua vichwa kama wewe si mtampinga na kumwaibisha? kwa nini asichague mzee wa ndio mzee?

how can u plan for the future while you wont b there?? \\

chib said...

@ Kamala :-))

Anonymous said...

Kwanza naomba kuuliza nini maana ya kustaafu?

Jumaa said...

Maana ya kustaafu ni pale mtu anapochoka kimwili, kiakili na kifikra kuendelea kufanya kazi ya kulipwa mshahara. Wakati huo huendelea kula, kutoa ushauri na kusubiri kifo tu!!