Member of EVRS

Tuesday, 7 December 2010

Tuwe Waangalifu na Mwisho wa Matumizi ya Bidhaa

Mimi bado nina imani vitu vinavyotengenezwa Bongo, vina uzuri fulani, na kwa kiasi fulani huwa vina ubora unaoridhisha hususan mambo ya vyakula.
Ninaogopa kuvamia hasa vile vinavyotoka Uchina, kwani vingi huwa ni bandia. 
 
Lakini wabongo wanaudhi pale wanapokuwa si makini katika kuangalia mazao yao wanayouza au kununua kama yana vigezo vyote vinavyofaa kwa mlaji kupata taarifa sahihi ya vyakula vyenyewe, kama paketi au gunia limefungwa vizuri, bidhaa iliyomo ndani haijaharibika, na kama lebo inaendana na bidhaa iliyopo. Na cha muhimu zaidi tarehe ya mwisho ya matumizi ya bidhaa yenyewe. Hapo mii ndio hutoa jicho la nguvu. 
  
Nikiwa mitaa yangu ya huku, nikisikia mtu aja kutoka Bongo, ni kawaida yangu kuagiza chochote ali-mradi nafsi yangu itafurahia matunda ya mamaland, hata kama ni vitumbua, wee leta tuu.

Kwa mara nyingine tena nilikutana na lebo hii hapo juu, tarehe ya mwisho wa matumizi, nimeitafuta kwenye kalenda zooooooote sijaipata. 
  
Hivi hao watengenezaji wa vyakula hivyo, huwa hawana elimu ya tarehe za kwenye kalenda, na hao wanaonunua kuuza vyakula kwenye masoko haya ya kisasa hawana wataalamu wa vyakula kukagua kama kila kitu kiko sawa.  
   
Ukisiskia mtu anasema bidhaa za wabongo ni feki sijui utamjia juu au uta.... 
  
Tunahitaji kuwafahamisha wajasiriamali wetu kuwa makini na bidhaa zao kama wanataka mafanikio ya kweli.

3 comments:

EDNA said...

Kaka umenena

SIMON KITURURU said...

Tarehe 30 mwezi wa Pili 2011 labda kwa kalenda tofauti na tutumiazo!


Ila mimi naamini Wabongo wengi huwa hawaangalii tarehe za kuexpaya kitu!:-(Si hata katika nguo- Mitumba kwetu ni brandi nyuu tu?

emu-three said...

Wanasema wabongo chakula kina-expire tumboni...lol