Member of EVRS

Saturday 20 February 2010

Mashambulizi ya Mabomu Kigali

Jana jioni Katikati ya mji wa Kigali kulitokea tukio la watu kurusha mabomu ya mkono na kusababisha mtafaruku katika kituo cha mabasi yanayotoa huduma mjini.

Muda yaliyotupwa na kulipuka, kwa kawaida huwa na msongamano wa watu wengi sehemu hiyo wakitokea kazini kuelekea nyumbani.

Inasemekana kuna watu wawili waliokufa papohapo na wengine kadhaa kujeruhiwa na kupelekwa kwenye hospitali kuu ya Kigali kwa matibabu.

Bado wahusika halisi hawajajulikana isipokuwa inahisiwa ni wapiganaji waasi huenda ndio wakawa wamehusika.

Tukio hili halikujulikana sana kama limetokea sehemu nyingine za mji wa Kigali, na shughuli zilikuwa zinaendelea kama kawaida ikiwa ni pamoja na kazi hata na kumbi za starehe kama ujuavyo ni wikiendi.

Nikipata habari zaidi zilizothibitishwa nitawajulisha.

4 comments:

Anonymous said...

Poleni sana kwa msukosuko huo, ni furaha k ufahamu kuwa mu wazima.

Fadhy Mtanga said...

poleni sana kwa kadhia hiyo. duwa zetu ni kuzidi kwenu kuwa salama.

mumyhery said...

Poleni sana tunashukuru kusikia mmenusurika

chib said...

Tunashukuru mji wote ulikuwa shwari mchana wote na watu wanaendelea na kazi kama kawaida.
Taarifa niliyoipata ni kuwa kumbe yalipigwa usiku wa manane.
Kwa sasa hapa Kigali ni usiku na ninaona helikopta zinazunguka angani kwa sasa labda kuhakikisha usalama.
Watu wanawafananisha hao warushaji wa mabomu kama vibaka tu!!