Member of EVRS

Saturday, 20 February 2010

Mkoa wa Mara Kulikoni!!!

Ni majuzi tu Mkoa wa Mara umezika wananchi 17 wa ukoo mmoja waliouawa kikatili kwa sababu ambazo zinasadikiwa ni masuala ya kulipiza kisasi.

Kisa hiki kimewaudhi sana watanzania wengi na hata watu wanaojali umuhimu wa maisha.
Watu walipata simanzi baada ya kuona hata watoto wasio na hatia wameuawa kikatili.

Sasa tena kuna mpya, Mtu mmoja anayeshukiwa kushirikiana na wezi huko Tarime ameuawa na kisha kuchomwa moto, na kama hiyo haitoshi, wamechoma nyumba zake zote 7 ikiwa ni pamoja na ghala la chakula.

Ilibidi mtoto wake mmoja wa kiume atimue mbio baada ya kuona umati mkubwa ukiivamia nyumba yao wakidai wanakuja kumsaka mwizi!!

Mkoa wa Mara, vipi tuuhamishie Somalia au Afghanistan nini?

8 comments:

Anya said...

Hi
My translater doesn't work :(
I cannot read your post !!!

Have a wonderful sunday

Anya :-)

Anonymous said...

Hii ni taarifa mbaya sana, huu mkoa kwa sasa unaongoza kwa idadi ya watu wanaouana kwa sababu ya malipizi na visasi, na mara zote visasi havina mwisho hadi kiteketee kizazi kizima. Hii ni mbaya sana. Tunahitaji nguvu kamili kuingilia kati suala hili la sivyo litasambaa kama gugu linavyosambaa ziwani na kuharibu ziwa zima. Hii ni indiketa.

EDNA said...

Hawa watu sijui wana matatizo gani,Inasikitisha kwa kweli.

chib said...

Thanks Subi and Edna for contributions
@Anya: There is no google translator for Swahili language. I will translate by giving an english version, or I will send to your mail/blog, but it is a very sad story

mumyhery said...

kuchinjana kama mbuzi, kama kweli ni visasi inatisha!!!

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli inasikitisha sio uongo. Sijui tumekosa nini sisi wanadamu au ndo mwisho wa dunia.

Anya said...

Thanks for the translation
Yes its a very sad and touching :(

Anya said...

Thanks for the translation
Yes its a very sad and touching :(