Member of EVRS

Wednesday, 17 February 2010

Tangazo la Mkutano Mkuu wa Watanzania wanaoishi Jimbo la Gauteng, Afrika Kusini

Tunapenda kuwatangazia watanzania wanaoishi katika miji ya Johannesburg na Pretoria kuwa kutakuwa na mkutano mkuu wa jumuia ya watanzania wanaoishi jimbo la Gauteng siku ya Jumapili ya tarehe 14.03.2010.

Mkutano huu utafanyika Kempton Park Civic Centre, makutano ya barabara za CR Swart Ave na Pretoria Road, Kempton Park, Johannesburg kuanzia saa nane mchana.

Pamoja na kujadili mambo muhimu ya jumuia hii, tunatarajia kupitisha katiba na kuchagua viongozi wa jumuia.
Kuhudhuria kwako ni muhimu katika kufanikisha shughuli hii. Ukipata ujumbe huu, tunaomba usambaze taarifa ya mkutano kwa watanzania wengine unaowafahamu.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na kamati ya maandalizi kwa barua pepe (watanzaniagp@gmail.com) au kwa simu zifuatazo:
+27799965120
+27835 566966
+27791035599

Karibuni sana
Kamati ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Jumuia ya Watanzania Gauteng

Maombi kutoka kwa Faustine

1 comment:

Anonymous said...

Ahsante kwa taarifa