Member of EVRS

Sunday, 7 February 2010

Jamani! Ebu Tuwe "Serious" Kidogo


Wikend iliyopita nilienda Dar Kusalimia ndugu jamaa na marafiki. Muhimu kuliko yote ilikuwa kusalimia familia.
Wakati naondoka nilipewa zawadi ya keki i kiwa kwenye vipande vidogovidogo na ikiwa imefungwa kwa unadhifu kabisa.
Nilipofika Mtaani kwangu huku, niliitoa, kwa mshangao nilikuta imeandikwa tarehe ya mwisho wa matumizi kuwa ni 31 Februari 2010. Nasema nimeshangaa kwa sababu najua mwezi wa Februari huwa ni mfupi, ukizidi sana unakuwa na siku 29. Na kamwe hauna tarehe 30 au 31!
Pamoja na kuwa keki hizi zilikuwa nzuri sana, lakini zinaweza kumtia wasiwasi mlaji kwa kutokuwa na imani ya ubora au mtengenezaji.
Wanasema kwenye masuala ya misosi hakuna dogo...
Gonga picha kama unataka kuona kwa uwazi zaidi hiyo tarehe.

7 comments:

Simon Kitururu said...

Hii kali! Kampuni hiyo yatumia kalenda tofauti nini na tuzijuazo?


Lakini wengi twatokea katika mazingira ambayo kipimo cha siku maharage hayafai ni KUONJA na maharage hata ya mwaka juzi yatalika ilimradi UKIYAONJA kiladha hayajachacha.:-(

Kwahiyo Mkuu ukiigina ladha yake kama tamu basi hiyo keki ni Mswano tu.Au?:-)

Na ukiwa na wasiwasi nayo hata kama haina kasoro waweza ukaumwa tumbo la hofu!:-(

chib said...

Mkuu, mie nilishazifuta zote, na wala hata muungurumo wa tumbo hakuna.

Faith S Hilary said...

Hahahahahhahahahahahhahahahahahahhahaa!! kumbe umeshaila!!! gosh! naitaka hiyo keki inayo-expire tarehe 31 february lol

Fadhy Mtanga said...

Mtakatifu Simon umesahau kuwa huku injini watu tunatambia 'expire dates' kwa kuonja ladha. Wakati mwingine ladha inakuwa tayari kimeo lakini tunalazimisha kingi kwa sababu itaharibu uchumi wa familia kama itamwagwa.
Candy nawe waitaka?
Ila mkuu Chib ukaamua kuifukia vivyo hivyo. Uitupe ili iweje? Bila shaka ilikuwa tamu tamu tamu balaa!

Halil Mnzava said...

Hiyo ndiyo Bongo darisalama!!!

Faustine said...

Bongo watu wanaishi kwa kudra za Mwenyezi.....

Mzee wa Changamoto said...

Nilianza kucheka lakini nilipowaza zaidi nikafikia mahala kujiuliza NI WANGAPI WAMEKULA VYA NAMNA HIYO AMBAVYO NI UOZO ZAIDI YA ITAKIWAVYO?
Tunacheka tukisikitika lakini hali ni mbaya kuliko maelezo.
Pole Kaka.
Mie zangu sala za kila siku kwa WENZETU WALISHWAVYO NA KUISHISHWA WASIVYOSTAHILI.