Member of EVRS

Tuesday, 23 February 2010

Chemsha Bongo kwa wenye IQ Ndogo tu!

My house is in a little bit mess

Plumber is busy overhauling the old system in some places and put new, and painter is standby to start his part....I cant get enough time to settle and read news from various blogs!!!

I hope soon I will be okay!

Lakini nina chemsha bongo ya vilaza, sihitaji majibu, lakini ukiona umekwama hata neno moja tu, naomba ukajisajili kwenye chama cha vilaza!

Si unajua wanamsingizia paka kuwa ana roho saba!! Taja maana tofauti 7 za neno Paka

Katika maneno yafuatayo taja maana au matumizi 5 za kila neno
Ganda
Panda

Mwisho... matumizi 15 tu ya kioo, tahadhari: matumizi utakayotaja yasishabihiane

9 comments:

Anonymous said...

Chib, naomba ufunguo wa chumba cha vilaza nimpatie M/Kiti nataka kujiandikisha chap chap nimalize hili zoezi. IQ yangu ni negative.

1. Ganda - Kitendo cha kuganda kitu
2. Ganda - Msemo wa kisasa kumaanisha, 'subiria'.
3. Ganda - Ngozi ya tunda
3. Ganda - Kasha la risasi
4. Ganda - Neno linalotumika kwa lugha ya Kiingereza kumaanisha watu wa asili ya Uganda
5. Ganda - Jina la mtu

PANDA
1. Panda - kuotesha au kusia mbegu
2. Panda - kukwea kimo fulani kwenda juu mfano mlima au mti au gari
3. Panda - jina la kampuni ya utengenezaji king'amuzi virusi katika tarakilishi
4. Panda - jina la mnyama
5. Panda - jina la mgahawa

KIOO?
1. Kioo - kifaa cha kuweka dirishani (nyumba, gari)
2. Kioo - kifaa cha kutizamia pembeni mwa gari
3. Kioo - kifaa cha kujitizamia sura
4. sijui....
5. Hiyo hiyo...

15. Naomba ufunguo wa kuelekea Vilaza Room.

Fadhy Mtanga said...

Kaka Chib wakati nasubiria funguo ya VILAZA room nikaungane na da Subi, ngoja nizuge na tujibu twangu twa kilaza.

Maana 7 tofauti za neno PAKA:
1. Mnyama mdogo afugwaye.
2. Eneza kitu cha majimaji ama laini juu ya kingine.
3. Weka rangi katika ukuta, gari nk.
4. Dhalilisha.
5. Naniliu.
6. Deshi deshi
7. nikupe mji?

Matumizi 5 ya Ganda
1. Sehemu ya nje ya tunda.
2. Sehemu ya nje ya risasi
3. Geuka kuwa barafu.
4. Fanya kitu kiwe kigumu.
5. Nata ama shika mahali.

Matumizi 5 ya Panda
1. Mgawanyiko ktk kitu km njia ama mti.
2. Paji la uso.
3. Enda kuelekea juu ya kitu km mlima ama mti.
4. Ingia katika chombo cha kusafiria.
5. Weka mbegu au mche ktk ardhi ukuwe.

Matumizi 15 ya Kioo.
1. Kitazamia.
2. Kujitazamia.
3. Mapambo
4. Madirishani
5. Kutengenezea vyombo vya nyumbani
6. Vifaa vya maabara
7. Kutengenezea vifaa vya elekroniki
8-15 ntadanganya bure!

Naenda zangu vilaza room lakini marks zake uniletee.

chib said...

Da Subi na Kaka Fadhy....Ingekuwa bora kama ningetoa zawadi kubwa kabisa kwenye chemsha bongo hii. Mmenichekesha mpaka ufunguo wa chumba cha vilaza nimeupoteza, nawaweka kwenye kundi la wabunifu, ha haa haa

Faustine said...

....Heri mimi ambaye sikujaribu!...

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

I wishi ningekuwa na IQ ndogo kujaribu.

natumaini Chib ni kilaza zaidi kulikovy vyote vilivyojaribu hapa na ndo maana akapoteza funguo za Vilaza wenzie!

pandana!!!!!!

Mija Shija Sayi said...

Chib ndo nini sasa? vilaza tuko wengi ngoja kwanza nijipange ndo nije kuomba funguo kama zitakuwa zimeshapatikana...

Mmenichekesha leo.........duh.

mumyhery said...

naomba namba ya usajili !!!

Fadhy Mtanga said...

Kaka Chib zawadi ni mi na da Subi. Angalau tumejaribu!

Anonymous said...

I seldom leave comments on blogs, but you really impress me, also I have a few questions like to ask, what's your contact details?

-Johnson