Member of EVRS

Wednesday, 17 June 2009

Ukali wa Mabosi Kazini!

Nataka kujuaaa….

Kwa nini maofisini mabosi wanapokuwa wakali sana katika kazi, wafanyakazi wengine hawakosi sababu za ukali huo!!!

Kama bosi ni mwanaume aliyeoa, utasikia watu wanasema, aaah.. huyo kakokorofishwa na mamsap huko nyumbani kwake, kwa walioshindwa utakuta wanasema, kama ni ukali wake, aupeleke huko kwa mkewe!!!, sasa huyo mke ndio shock absorber?!!
Kama bosi ni mseja (bachelor), basi utasikia, m#h*, ebu mtafutieni mke.., mtaona ameufyata!!! Mke huyo huyo tena anapoza mambo!!!

Kama bosi ni mwanamke na ameolewa, utashangaa utengano sasa, wanawake watadai .. wajua eeh, wanawake hatupendani.., iwapo bosi hajaolewa au hana mtoto, basi utasikia, mwee, hayo ni mafrastraa tuu (frustrations). Au wakati mwingine utasikia, huo ni wivu tu, ameona nimetia pamba za nguvu kuliko zake basi ndo kelele!!!
Kwa upande wa wanaume, kwa bosi mwanamke mara nyingi huwa hawana komenti nyingi!

Upo hapooo!!!

9 comments:

Anonymous said...

Tatizo ni kuwa watu wengi ni wavivu, kwa hiyo wanatafuta visingizio mbalimbali vya kuhalalisha uvivu wao. Mabosi mara nyingi wako sahihi!

Fadhy Mtanga said...

Mi nadhani ni kwa uvivu wetu nd'o maana hatuishiwi sababu kwa ukali wa wakuu wetu wa kazi (mi huwa situmii neno bosi)
Lakini pia wakuu wengine wana mambo, tena siyo madogo.
Ni hayo tu kaka!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wewe Anonymous lazima utakuwa bosi mkorofi.

mimi sina bosi, bali mimi ni bosi wangu mwenyewe.

eti mu wavivu? kama wavivu mbona kampuni haifi?

nikasumba ya mabosi kufoka utadhani wanaweza kila kitu. kuna saikolojia mbovu kuwa wafanyakazi lazima watishiwe ili kazi iwe njema. wengine hudai kuwa bila ukali kazi haiendi.

niliwahi kufanya kazi sehemu, bosi alikuwa mzungu, alileta ukali nikaandaa mgomo, mgomo wenyewe ulikuwa wa kuacha kazi bila malipo kwa kisingizio cha ukorofi wa bosi. mbona tulibembelezwa nakuongezewa mshahara? unajua kwa nini> ili ufanye kazi ile ilikuwa ni lazima upata mafunzo lasimi kwa miezi mitata na uzoefu. kwa hiyo kuacha kazi basi inamaana hakuna kazi na kila kitu cha simama.

sijui!

Yasinta Ngonyani said...

"wengine hudai kuwa bila ukali kazi haiendi." Bado tupo pale pale pa kupiga watoto au kumpiga mtu kwa maneno. kaka Chib hayo uliyoyasema hapo juu yanaweza kuwa 50% ni kweli. Na pia sasa imekuwa kama mila na desturi yaani kuonyesha ile mipaka nani ni bosi na nani ni mfanyakazi. Pi kumbuka bosi naye ana bosi labda anakuwa amekaripiwa na bosi wake pia. Sijuilakini ila ni wazo tu.

chib said...

Nakubaliana na maoni ya kila mtu, kwani matatizo yanaweza kuwa upande wowote wa mkuu mwenyewe au watendaji wa chini yake.
Nashukuru kwa mawazo, kweli yanapanua uwigo wa uelewa

Anonymous said...

Mimi si bosi Kamala, nasimamia ka kitengo kadogo chini ya mabosi lukuki, ukifuatilia chain yao, mimi sina kitu

jaz@octoberfarm said...

hi chib...what an interesting trip you had. i can imagine it will take a while to have it all sink in! so glad you are back safely and hope you catch up on your sleep. i never had trouble with jet lag going places. it always hit me on my return. joyce

jaz@octoberfarm said...

you have given me such a better way to describe jet lag....a body and mind crash!! that is sooooo much better and visual as well! joyce

Simon Kitururu said...

Kuna uwezekano hawa mabosi ni wakali hata nyumbani nawafahamu baadhi ambao kazini wanakoroma na wakirudi nyumbani mama watoto na watoto wanafyata mkia!
Na ni kwa kimada tu au kwa kipoozeo ndio unakuta wamepoa na stori nyingiii!

Kwa bahati mbaya sio mabosi wengi niwajuao kazini na wakiwa nyumbani lakai!:-(