Member of EVRS

Monday 27 September 2010

Kenya Airways: Nao Wamo Kwa Ndege za Mitumba


 Nilikuwa kimya kwa siku kadhaa, kwani nilikuwa mimekabiliwa na majukumu yanayohusu mipango ya maendeleo na utoaji huduma za macho, mpango huu unahusisha juhudi binafsi za wananchi wazalendo na wazawa katika ukanda wa Afrika Mashariki, na kwa kuanzia, Kenya ndio imekuwa ya kwanza kuratibu mpango huu kwa nchi shirikishi za umoja huu wa kanda ya Afrika Mashariki.
Kwa kuwa nilikabiliwa na zaidi ya masaa 40 bila ya kulala kutokana na usafiri kuanza saa 6 usiku na kuondoka usiku wa manane ilhali mkutano ulikuwa unaanza saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku, na baada ya hapo kuandika muhtasari.. hakika siwezi kusema zaidi........



kusafiri, ni kuona mengi na pia kujifunza mengi. Hapo jana wakati narejea Kigali, nilipokuwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi, niliona ndege kwa mbali, nikadhani ni ya KLM, lakini kwa kuwa nimezoea kuona madege ya KLM ambayo huja huku, nikashangaa kwa nini safari hii wameleta ndege ndogo, tena jioni.. ..... wakati huwa zinatua huku usiku na kuondoka usiku huo huo..... nikawa na maswali...


Kusoma jina la ndege likawa halifanani na rangi ya ndege niliyoizoea!, nilihisi bado nina usingizi, na hivyo rangi zikawa zinanichanganya. Nilipata moyo baada ya kuona kuna baadhi ya wasafiri wenzangu nao walikuwa wakishangaa kama mimi. Wengine walikuwa wakikenua meno na kucheka, kwani nao naona walikuwa wanshangaa hizo rangi za ndege kuwa ni za KLM wakati shirika linaloimiliki ni Kenya Airways

Tukutane tena wakati mwingine, kwani safari hii ilinifurahisha kwa mengi ambayo iliniwezesha kukaa miji mitatu, kwenye nchi tatu tofauti kwa siku moja!!

5 comments:

emu-three said...

Aisee mitumba mapaka kwenye ndege..mmh, haiwezi kuwa hatari baadaye, manake tunaweza kuletewa mitumba ya Ubongo...

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Vipi ulipoingia ndani, ndege ilikuwaje? Huduma zikoje? Kama ni mtumba kwa rangi tu lakini kwa ndani mambo yako sawa si neno.

Nadhani hii inatokana na ushirikiano wa karibu kati ya Kenya Airways na KLM ingawa pengine ningetegemea tu nembo fulani ndogo ya KLM kuwekwa mkiani. Lakini rangi ndege nzima duh!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Ukistaajabu ya wabongo utaona na ya watani wa jadi pia....lol!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

...bila shaka ushasafiri na Precisionair ile boeing 737 yao. Imepakwa rangi za PW lakini ndani ni KQ....lol!

Mija Shija Sayi said...

Nijuavyo mimi ni kama alivyosema Matondo. Hawa ni wamoja, ila sio sababu basi ndege nzima kupakwa rangi ya KLM.