Member of EVRS

Sunday, 19 September 2010

Watoto walemavu wa Tanzania Watumika Kama Kitega Uchumi Kenya

Juzi jioni mtanzania mmoja ambaye anaishi jijini Nairobi kwa muda mrefu sasa aliyejulikana kwa jina la Yohana Kulwa pamoja na mkewe raia wa Kenya walikamatwa na makachero wa Kenya baada ya kugundulika kuwa alikuwa anawatumia watoto walemavu kutoka Tanzania kama mradi wa kujipatia kipato.

Watoto hao wadogo chini ya miaka 10, wamekuwa wakichukuliwa na gari kutoka nyumbani kwa Yohana saa 10 alfajiri mpaka katikati ya Jiji la Nairobi, na kisha wanapakiwa kwenye mkokoteni ambao huanza kuwasambaza sehemu mbalimbali za Jiji la Nairobi ambazo zinapitwa na watu wengi.

Watoto hao hukaa wakiomba kuanzia asubuhi mpaka jioni bila hata chakula, ikifika muda wa saa 9 alasiri, wengi huwa wamechoka sana na njaa, na hivyo kupitiwa na usingizi, ukizingatia huamshwa mapema karibu ya saa 9 usiku.

Ifikapo jioni, watoto hao hujisogeza taratibu kwa kujivuta barabarani hadi kwenye sehemu ambapo gari hilo huja kuwachukua.

Watu walio kwenye mtandao huo, huwa wajanja, kwani jioni uhakikisha ya kuwa mwendesha mkokoteni yupo karibu, ambapo hutumika kukinga watu wasione hao watoto wanapopakiwa kwenye gari na kurudishwa kwa tapeli huyo wa Kitanzania na mkewe.

Siku polisi walipowafuatilia walimkuta mtanzania huyo na mkewe wakiwa wanagalia runinga kwa starehe zao, huku walemavu wao wakiingizwa ndani mmoja mmoja.

Polisi walipohesabu pesa walizoingia nazo hao siku hiyo, walipata jumla ya KSh zaidi ya 13,000 (Karibu ya dola za marekani 150), na inasemekana kila siku watoto hao huja na kiasi kama hicho.

Uchunguzi wa polisi bado unaendelea, na inatarajiwa wezi hawa watafikishwa mahalamani wiki ijayo.

Wakati huo huo, polisi wa Kenya, jana wamekamata watu wengine tena ambao hutumia chokoraa pia kwa mtindo huo huo kwa kuwatumia kama nguvu kazi, tofauti ni kuwa watoto hawa sio walemavu, na walikutwa na jumla ya zaidi ya ksh 2,000 kama makusanyo ya siku hiyo ya jana.

Kwa mtazamo wangu:
Huyo mtanzania anatakiwa kupata adhabu kali, si ajabu aliwachukua watoto hao toka kwa wazazi wao kwa kuwadanganya ya kuwa anawapeleka kusoma au ....., kumbe ni tapeli mkubwa

NB. Watoto hao walionyeshwa kwenye runinga ya Citizen tangu wanachukuliwa na gari dogo asubuhi, kubebwa kwenye mkokoteni, wakiwa kazini, jioni walipokuja kuchukuliwa na mwisho wakati Mtanzania huyo alipokamatwa na mkewe. Na matapeli hao walikiri kufanya mchezo mchafu huo.

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni jambo la kusikitisha sana na Mungu awalaani kabisa na hiyo adhabu watakayopata iwe kali,kali kali mno. Huu sio ubinadamu kabisa.

SIMON KITURURU said...

:-(

Juma said...

Sikutegemea kama kuna mtu anaweza kuwa mnyama kiasi hicho, yaani kugeuza ulemavu wa mwingine kuwa dili kwake

emu-three said...

Sasa katika hali hii unatgemea kweli `tumuombe mungu atusikilize maombi yetu...?'
Atatuuliza `mbona mlikuwa mkinidhulumu haki yangu, kwasaabbu mlipomdhulumu mja wangu ni sawa na kunidhulumu mimi, sasa kwanini mnalia kuwa siwasikilizii dua zenu...'
Dunia hii inavurugwa na wengi, sasa hivi mayatima hawathaminiwi, mali yao ya halali inaliwa na wajanja. Haya hata wasiojiweza wanadhulumiwa? Utashangaa maenijioo, yameanzishwa kwa mlango wa kusaidia hawa watu, lakini ni nani anayeneemeka na hiyo misaada...utagundua kaducho kwa wanaotakiwa kuneemeka na donge nono kwa `mshikaji...'
Samahani, sio kwamba nona donge...tutahukumiwa kwa dhuluma!

EDNA said...

Dunia inaelekea wapi jamani?