Member of EVRS

Wednesday 15 September 2010

Kampeni za Uchaguzi 2010 Tanzania

Habari hii nimeitoa kwa mwanablogu kijana, Upepo Mwanana ambaye anatarajia kupiga kura yake kwa mara ya kwanza mwaka huu. Na huu ndio mtazamo wake:

Nimekuwa nikfuatilia kampeni za siasa, kwani sitaki kufanya makosa wakati utakapowadia wa kumchagua kiongozi wangu wa baadaye, ukizingatia ya kuwa hii itakuwa ni mara yangu ya kwanza kushiriki katika zoezi zima la kupiga kura za kuchagua viongozi wa nci yetu,

Nimekuwa nikisikiliza kwa makini sera za wagombea mbalimbali na kuzipima kama zina ukweli, ushawishi, na pia kuangalia kama kweli zinatekelezeka au ni changa la macho.

Nahisi naanza kukata tamaa, kwani wanasiasa au wagombea nafasi za kisiasa badala ya kuhubiri sera za vyama vyao, wamekuwa mstari wa mbele kusikiliza mwenzie alisema nini, na wao kusema ya kwao kutokana na wengine walichosema hapo awali, na mwisho hakuna kampeni tena bali ni kupeana vidonge na kujibu mapigo!!!!!

Sie tunaotaka kupima sera tumejikuta tukipima nani ni bingwa wa kujibu mashambulizi, na mara ,,, hatimaye zoezi la kupiga kura litafika.. sasa hapo tutampigia kura nani?, nahisi hatutakuwa tumempata kiongozi atakayekidhi tulichotaka kusikia kabla ya kuamua.

Mpaka sasa mimi naona wengi ni wahuni na matapeli tu. Wanabembeleza wachaguliwe kwa matakwa yao binafsi. Na kwa maono yangu, naona vyama vimeelekeza nguvu na pesa nyingi kwa wagombea urais, kwani kutumia helikopta nyingi na magari utitiri kwa mgombea mmoja, wakati wagombea ubunge na udiwani wakiswaga lami ni kuonyesha ishara ya uchoyo na unafiki tu

HATUDANGANYIKIIIIIII

3 comments:

Fadhy Mtanga said...

mie nishajua nitamchagua nani...ntakuwa napiga kura kwa mara ya tatu...mara mbili zilizopita nilipiga kura kwa ushabiki..
mwaka huu.....hapana... nimeshafikiria sana. nitaitumia kura yangu vema.

Anonymous said...

Hongera Fadhy Mtanga kwa kubadilika na kutambua ukweli na maana ya kupiga kura.
Tupo pamoja

chib said...

Joto ya jiwe...:-)