Member of EVRS

Monday, 6 September 2010

Kagame aapishwa kuwa Rais wa Rwanda

Rais Kagame wa Rwanda ameapishwa leo kuwa Rais kwa muhula wa pili.
Sherehe hii ilihudhuriwa na viongozi wa nchi mbalimbali kutoka nchi kadhaa za kiafrika.
Baadhi ya viongozi hao ni kutoka Burkina Faso, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Afrika ya Kati, Kenya, Malawi, Ethiopia, Liberia n.k.


Kagame akila kiapo leo.
Rais Kagame akisaini hati ya kiapo huku aiangaliwa na jaji mkuu wa Rwanda Aloysie Cyanzaire


Gwaride lililokuwa limeandaliwa mahsusi kwa shughuli ya leo kwenye uwanaja wa Amahoro.


Katika hotuba yake, Rais Kagame aliwashukuru viongozi wa kiafrika kwa kukubali mwaliko na kuonyesha mshikamano wao. Pia aliwashukuru wanyarwanda kwa kuchagua serikali ambayo wanaona itakidhi matakwa ya maendeleo ya wanyarwanda.
Lakini alikemea vikali tabia za baadhi ya mashirika ya kimataifa na haki za binadamu kwa kuamua kwa makusudi kupotosha ukweli wa amani iliyopo Rwanda, na kuamua kutangaza propaganda za uongo kuhusu hali iliyopo Rwanda kwa sasa.

Alionyesha kushangazwa kwa mashirika hayo kutozingatia hali halisi ya kisiasa ya Rwanda katika kipindi hiki cha mpito baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Mwisho alisisitiza ya kuwa hakuna maendeleo yanayokuja bila kuwa na demokrasia (Hiki ni kijembe kwa wale wanaoisifia Rwanda kuwa na maendeleo makubwa sana na huku wakisema hakuna demokrasia kabisa). Na aliyakemea mashirika hayo kuwa yanataka kuchochea gurudumu la umaskini na maendeleo duni kwa nchi zinazoendelea kama Rwanda ( Perpetuates cycle of poverty and underdevelopment).

Alionya ya kuwa Rwanda kamwe haitakubali kuamriwa cha kufanya kama Taifa, akiwa na maana utaifa na mahitaji ya Rwanda ndio yanayopewa kipaumbele.


Quot from Kagame: A successful society, achieves National cohesiveness and common interests.

Hotuba hii ilinigusa sana, hasa ukizingatia juzi nimepokea taarifa ya kuwa kuna mashirika tajiri, eti kwa kuona kuna uhaba mkubwa wa madaktari wa fani fulani za magonjwa katika nchi za kiafrika, basi wanataka kuelekeza misaada yao ambayo walikuwa wakiitoa kwa kutoa mafunzo kamili ya udaktari kwenda kuwafundisha watu watakaowaokota mitaani na kuwapa mafunzo mafupi ya kutibu watu ikiwa ni pamoja na upasuaji ili waongeze idadi ya "madaktari" wa fani hizo katika nchi za kiafrika. (J*^ga kabsaaa)
Nikiwa mmoja wa wadau katika fani hizo zenye upungufu, tuliombwa kutoa mapendekezo kama kipima joto, ingawa wao ati walishakubaliana. Nahisi joto wamekwishalipata.

Picha kutoka Kagame fan club

4 comments:

Subi said...

Huo ushauri wa kuokota watu na kuwapa mafunzo ya upasuaji kisha kuwaruhusu watibu binadamu, naomba nikusaidie kutamka bayana kuwa huo ni UPUMBAVU mkubwa kabisa. Afadhali ujinga huwa unaelimika, kuliko upumbavu huu wa kuwaamulia Waafrika na kuwalazimisha wakubaliane na mambo haya. Hivi wangekubali hili lifanyike kwao? Kuonesha wanajali kumbe wanadhihirisha jinsi wasivyojali.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mimi naona ni sawa tu! kwani nani aliyeamua kuwa Chibuga lazima asome wee ndo awe dokta si wadhungu?? sasa wana hakai ya kuamua vinginevyo

harafu kuna watu wanatibu bila taaluma

oye

John Mwaipopo said...

hii mutusi inaonyesha inafanya kazi, haichekicheki hata pasipofaa kucheka.

John Mwaipopo said...

hii mutusi inaonyesha inafanya kazi, haichekicheki hata pasipofaa kucheka.