Member of EVRS

Friday, 3 September 2010

Vurugu za Mikate Msumbiji!


Juzi usiku nilikuwa naangalia TV Mozambique kupitia satellite dish.

Kwa kuwa sielewi kireno, nilibaki nikishangaa kuona watu wanaume kwa wanawake tena wa rika zote wakivamia maduka na kuiba kila kitu kilichokuwepo, na huku barabarani vijana wa kiume wakichoma matairi ya magari.

Nilimshuhudia dada mmoja labda akiwa kwenye miaka kama 20 hivi akitoka na mabeseni kama 10 hivi kwenye duka lililovamiwa huku akikimbia akiwa na tabasamu usoni. Hakufika mbali kwani alivamiwa na kundi la vijana wa kiume wakiwamo na watoto kama wa miaka 12 – 13 wakampokonya mabeseni yote huku wakimwachia majeraha makubwa kichwani na usoni na huku akiwa tayari kagalagazwa chini.
Yote hii ilikuwa ni purukushani ya kumnyang’anya mabeseni ili na wao wajipatie. Kilichofuatia ni kilio na kicheko kikafutika kabisa usoni pake.

Pia niliwaona akina mama wa makamo na akina baba pia wakiiba unga kwenye duka la vyakula na kukimbia!

Jana ndio nikapata jibu kuwa waliamua kufanya fujo baada ya serikali ya Msumbiji kupandisha bei za vyakula. Lakini kilichowakera zaidi ni kupandisha sana bei ya MIKATE!!!

Polisi waliingilia kati na kufyatua risasi za moto. Vurugu hizi zimesababisha vifo vya watu 7 na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Pamoja na kuwa hali leo asubuhi imeanza kutengemaa kidogo, ingawa bado usafiri wa wananchi haujarudi sawasawa, serikali ya Msumbiji imetamka ya kuwa haitapunguza ongezeko la bei kama ilivyokuwa imeahidi jana kwamba itapitia upya.

Swali kubwa…. Tunaelekea wapi sisi nchi za Kiafrika? Je, sera za serikali zetu zina angalia hali ya wananchi kabla ya kufanya maamuzi au…?

Kwangu siamini kuwa suala la kupandisha bei ya mikate tu ndio inaweza kuleta vurugu kama hizi.

Habari za kina click here

Photo: By Reuters

3 comments:

SIMON KITURURU said...

Nahisi Msumbiji wanapenda mikate zaidi ya Bongo. Inasikitisha sana kuwa Afrika bado tunashindwa kujilisha pamoja na ardhi yote tuliyonayo. Tanzania yenyewe unaambiwa asilimia kubwa ya watu pamoja na amani zao hawashibi vizuri itakiwavyo kiafya.

Upepo Mwanana said...

Hizi njaa zitatuua

Anonymous said...

May life and time treat them kind and let things end in peace.


daily athens