Member of EVRS

Wednesday, 22 September 2010

Leo Katika Kona ya Siasa: Dr Faustine Ndugulile

Dr Faustine Ndugulile, wakati akitambulishwa na JK kwa wakazi wa Kigamboni siku ya uzinduzi rasmi wa Kampeni jimbo la Kigamboni


Dr Faustine akimwaga sera katika harakati za kuomba kura


Safari ya kugombea ubunge si kazi ndogo.  
Inahitaji maandalizi ya kutosha, uelewa wa hali ya juu kuhusu matatizo ya wananchi unaotaka kuwawakilisha, nia ya dhati katika kuyatatua matatizo bila kutanguliza maslahi yako binafsi na ahadi zinazotekelezeka. 
  
Kwani kipimo cha imani ya wananchi unaotaka kuwawakilisha, kitaoanisha ahadi zako na utekelezaji wake.
  
Safari hii ya kupata ridhaa ya wananchi pia inazua maadui kwa sababu mbalimbali zikiwamo tofauti za kisera na pia maslahi binafsi.   
  
Inahitaji moyo wa dhati, dhamira ya kweli na utashi wa kimawazo kutimiza matumaini ya watu. Na pia inahitaji uimara na msimamo thabiti katika ukweli unaouamini.  
  
Chagua mtu atakaye kufaa na kukuwakilisha vyema.  
   
Habari hii Imenukuliwa kutoka kwa mwanasiasa

2 comments:

SIMON KITURURU said...

Kila la kheri Dr!

Yasinta Ngonyani said...

Twakitakia kila la kheri kwa kweli!!