Member of EVRS

Sunday, 5 September 2010

Rwanda: Paul Kagame Kuapishwa Kesho Muhula wa Mwisho

Kesho, kutakuwa na sherehe ya kuapishwa kwa Paul Kagame kuwa rais kwa kipindi chake cha mwisho cha urais cha miaka 7. Hii ni kwa mujibu wa katiba ya sasa ya Rwanda.
Kwa ujumla Kagame bado anakubalika sana na wanyarwanda. Pichani juu: Katikati ya Jiji la Kigali kama linavyo onekana wakati wa jioni kutoka nyumbani kwangu.

Tangu mwezi wa nne, kumekuwa na marekebisho makubwa ya bararbara ikiwa ni pamoja na upanuzi kwa kuongeza njia mbili kwenye baadhi ya barabara ambazo zilikuwa na msongamano wa magari, na pia barabara zilizokuwa zimeanza kuonyesha dalili ya kuanza kuchakaa, hasa zile barabara maalumu zinazopita kwenye ofisi za balozi na wizara za serikali


Wajenzi ni wachina, lakini hawa sio wale feki, kwani wanafanya kazi kwa makini na kwa haraka, sio kama wale waliotengeneza barabara ya Sam Nujoma kule Dar es Salaam.

Wachina hawa, wana imani kubwa na sementi ya Tanzania, kwani katika ujenzi wa sehemu za wapita miguu, mitaro na kusimika nguzo za taa za barabarani wanatumia sementi pekee ya Twiga kutoka Dar es Salaam, Tanzania.Shughuli ya kuweka lami mpya ilikuwa inaenda sambamba na kuweka taa mpya na kuondoa za zamani, ambazo baadhi yake zilikuwa haziwaki, lakini wamebadili zote kabisa hasa barabara muhimu.
Kwa sasa barabara zimekamilika na wamemaliza kupaka rangi kingo za barabara ili zionekane kwa madereva kwa urahisi na pia kupanda miti na maua.
Kesho ni siku ya mapumziko, lakini nahisi jumanne nayo inaweza kuwa mapumziko iwapo watu watasheherekea sana kuapishwa huko kwa rais Kagame, kwani watu hupenda kukesha usiku kucha kwenye uwanja wa Taifa wa Amahoro, hivyo kushindwa kufanya kazi siku inayofuata.


1 comment:

Ivo Serentha and Friends said...

Good views, when they undertake the work means that the development goes ahead.

Hello Chib,good coming week,and thank's with the visit to "Travelblog"

Marlow