Member of EVRS

Thursday 16 September 2010

Chunga sana wezi wanaotumia Mtandao wa Mawasiliano

Maendeleo huja na raha Zake. Sula zima la mawasiliano limefikia hatua kubwa sana ya maendeleo, mawasiliano yanakwenda kwa haraka sana, na dunia imekuwa ni ndogo.

Mifano mzuri ni kama vile mitandao ya facebook, blogu, flikr, tweeter nk.
Unaweza kuwasiliana na mtu usiyemfahamu na mkawa marafiki bila hata kuonana au kujuana....lakini kila zuri huja na matatizo yake, suala la mawasiliano nalo halijaachwa nyuma

Kwa sasa mtandao wa mawasiliano umevamiwa na wezi (cyber crimes), ambao wamekuwa wakiwaaibia watu kwa mbinu mbalimbali.

Huko Kenya kuna dada mmoja ameibiwa jumla ya Ksh 100,000 (zaidi ya dola za kimarekani 1,000) kutoka kwa mtu aliyekuwa anajifanya anampenda sana baada ya kuwasiliana kupitia mawasiliano ya mtandaoni kwa wale wanaotafuta wapenzi wa kudumu (soul mates).

Dada huyo alikuwa akiibiwa kidogokidogo kwa kuwa kijana huyo alikuwa anamtumia ujumbe kuwa mara kakamatwa na polisi zinahitajika ksh 20,000, siku nyingine ati malipo ya hospitali, huku akijidai kuwa kwa wakati huo akiwa hana pesa, mpaka atoke hospitali nk. Na dada huyo alikuwa akimtumia pesa kupitia huduma ya M-Pesa akiamini anamtumia mpenzi wake kumuokoa na matatizo ya ghafla yaliyompata.

Kijana huyo mwizi, inasemekana ya kuwa alikuwa akikataa kumpeleka rafiki yake huyo wa kike mahali alipokuwa anakaa, na kwa sasa amepotea kabisa na wala hapatikani kwa simu. Kufika leo, ndio huyo dada akagundua ya kuwa ametapeliwa, na kimsingi ameishiwa na akiba yake yote aliyokuwa amejiwekea.

Nafikiri hili ni onyo kwa watu ambao wanakubali kudanganyika na wezi wa mitandaoni.
Chunga sana kuhusiana na watu ambao wanakuja na mahitaji ya pesa mtandaoni...

5 comments:

Fadhy Mtanga said...

pole zake dada huyo.

mie nimepokea barua pepe nyingi sana zilizoandikwa kiushawishi sana.

ni taabu tupu kizazi hiki. akili kumkichwa.

Yasinta Ngonyani said...

Ama kweli pola zake huyo dada!
Kweli mapenzi nayo yanaweza kumfanya mtu awe kipofu

Ahsante kwa ujumbe huu.

Yasinta Ngonyani said...

Ama kweli pola zake huyo dada!
Kweli mapenzi nayo yanaweza kumfanya mtu awe kipofu

Ahsante kwa ujumbe huu.

John Mwaipopo said...

luambo luanzo makiandi 'franco' aliwahi kuimba wimbo kwa kiswa-nglish cha harakaharaka 'mapenzi ya telephone.' analalamika kuwa amechoka mapenzi ya simu. anataka mapenzi ya kweli. kisicho machoni hakiko rohoni

hao wakina franco wamechoka mapenzi ya simu lakini kwa mtu anayemjua. inakuwaje mapenzi na mtu usiyemjua. tabia hii ya huyu dada inafaa kupewa jina lolote baya. ujuha, ujinga, umajinuni, upumbavu, ushamba, uwendawazimu n.k.

mie wala simpi pole!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mapenzi jamani