Member of EVRS

Tuesday, 14 September 2010

Furahia Mzaha: Mchagga Hapotezi Kitu


Mchagga alinunua mbuzi kwenye sikukuu ya idd...

Alipomfikisha nyumbani, akampa maelekezo mpishi wake
Nusu ya nyama ipike kwa ajili ya pilau, na itakayobaki itie kwenye friza!

Kichwa .. tengeneza supu na miguu fanya mchuzi chukuchuku!

Ngozi usitupe eeh, utaikausha na kuifanya mswala.

Utumbo, pikia na ndizi

Mifupa tutawauzia wenye mbwa, tena Massawe anao wawili na wamekonda kwa kukosa chakula.

Mafi yote kusanya na kupeleka shambani, hiyo mbolea.

Mpishi kwa kuona kakosa cha kwake, hata kwato...akamuambia bosi wake

Hutaki na sauti ya mbuzi tufanyie ring tone ya simu yako, mie naweza kutengeneza kwa alfu tu

Nashukuru mdau kwa kunitumia kisogeza siku!

picha pekee kutoka hapa

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kaazi kwelikweli hakuna kitu kupotea kweli wachagga ni kama wachina au?

Anonymous said...

ypmmualqmioawftfoice, justin bieber baby lyrics, ilmvyyl.

SIMON KITURURU said...

:-)

Fadhy Mtanga said...

nimecheka hadi nimeshindwa niandike nini

EDNA said...

hahahaa mbavu zangu,you made my day bro.

emu-three said...

Hahahhahahahhaha....we mbavu zangu zinauma..hhahhhhmmmmmmmmmh