Member of EVRS

Wednesday, 22 September 2010

Vituko Bongo: Mwanaume Mmbeya "Aolewa"

Bongo... kila kukicha hakuishi vituko

Kuna habari hii iliyoandikwa kwenye Global publishers ambapo mwanaume mmoja tena ambaye ana mke, amekuwa na tabia ya kuwapigia simu wake wa wanaume ambao anawajua pindi tu anapowakuta wamesimama mahali popote na mwanamke mwingine

Tukio hilo la aina yake lilitokea Septemba 17, 2010 Sinza ya Kumekucha jijini Dar es Salaam jirani kabisa na hoteli ya Lion ambako mwanaume aliyedaiwa kufanyiwa kitendo hicho anaishi.

Msafara wa magari ya kifahari yapatayo kumi na tano yaliwasili nyumbani kwa mwanaume huyo ndani yake kukiwa na waalikwa walioonekana kuwa na furaha za shamrashamra hizo.


Msafara huo ulipofika nje ya nyumba ya mwanaume huyo mwenye mke ulisimama huku matarumbeta yakipulizwa na watu wakiserebuka kwa ngoma ya Baikoko iliyokodishwa toka jijini Tanga.

Hata hivyo, ilidaiwa kwamba mwanaume huyo ambaye bado kijana alipochungulia nje na kuona wageni akiwemo ‘bwanaharusi’ aliingia mitini kwa kutumia mlango wa nyuma kwani toka jana yake alishanyetishiwa kuwepo kwa ‘ndoa’ hiyo ya aina yake.

Akiongea na waandishi wetu eneo la tukio, mmoja wa wageni waalikwa (hakupenda kutaja jina lake) alisema kuwa, wamealikwa katika sherehe ya ‘ndoa’ ya kijana huyo kwa lengo la kumshikisha adabu na kuachana na tabia yake ya ambea mtaani anakoishi.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kweli Bongo kuna vituko, ila hapo walimfanyia vizuri na nategemea amejifunza kitu. Watu bwana!!

emu-three said...

Vituko vya kukomeshana, kama ana tabia hiyo nafikiri atakuwa kajifunza kama ni mwenye kuelewa