Member of EVRS

Monday 31 August 2009

Watanzania: Ongeza ujuzi


Mdau wa blog hii Michael Mahande, kwa sasa yupo Jijini Bergen, Norway akichukua mafunzo ya shahada ya uzamili katika fani ya udaktari wa falsafa kwenye masuala ya epidemiolojia na takwimu (epidemiology and biostatistics).
Tunamuombea kila heri katika kipindi chote cha miaka 4 atakayokuwa huko Norway kimasomo.
Watu wananena... ukisoma sana ubongo unakuwa na kuzibana nywele kwa ndani, kwa hiyo nyingine zinapukutika, ila wahenga wanasema akili ni nywele, kila mtu anazo zake. Na ni kwa jinsi hiyohiyo, tafsiri za watu, ni kila mtu na yake!!!
Nimeshtuka, naachia hapa......

5 comments:

Anonymous said...

He huyo mtu kafika lini huko! Hongera mdau

Yasinta Ngonyani said...

Nakutakia kila la kheri ndugu yangu. Ila umeanza kipindi kibaya karibu baridi itaanza ila mambo yatakuwa pouwa!

Mzee wa Changamoto said...

Hebu ninukuu. "epidemiolojia na takwimu (epidemiology and biostatistics)."
HESHIMA KWAKO KWA HILI NA MASOMO MEMA MDAU

Asante Kaka Chib kwa kutuunganisha na waungwana wenye moyo kama hawa

Sarp said...

vizuri sana kuongeza juhudi.All the best mdau

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Wabongo Ubongo tunao, na japo mwanzoni masomo yanaweza kuwa magumu kutokana na tofauti za lugha, utamaduni na mengineyo, naamini kwamba utafanya vizuri katika masomo yako. Chapa kazi na jamii ipo inasubiri kufurahi pamoja nawe.