Member of EVRS

Thursday, 20 August 2009

Mafanikio ya soko la bidhaa za Tanzania nje

Majuzi nilimsikia waziri fulani wa Tanzania akisema soko la bidhaa za Tanzania na mauzo nje ya nchi kwa bidhaa hizo yalikuwa yameongezeka kwa takribani asilimia 30.
Habari hiyo ni ya kufurahisha kwa wananchi wote wa Tanzanai

Bidhaa za Tanzania kwa hapa Rwanda zina ubora wa hali ya juu kuliko bidhaa nyingi kwenye masoko. Kwa watu wanaotaka vitu kama magodoro bora, chakula chenye ubora kiwe kile cha kiwandani au fresh, basi hukimbilia kinachtoka Tanzania.

Lakini kwa kweli bidhaa za Tz ndio ghali kushinda nyingine. Ingawa watu wanasema kitu bora ni ghali...

Kilichonisikitisha hapa, ni kukuta kuna mkaa kutoka sehemu mbalimbali, lakini unaotoka Tanzania ndio ghali kuliko mwingine, na wale wanaotumia mkaa kwa nia ya kubana kidogo hununua mkaa huo, jambo nililokuwa najiuliza, hiyo miti ambayo huko Tz inakatwa kutengeneza mkaa wa kuja kuuzwa huku ni kweli kuna mingine imepandwa??
Sina hakika mheshimiwa waziri fulani alikjumuisha na uuzaji wa mkaa nje ya nchi kama sehemu ya majumuisho yake ya kuwa kipato cha kuuza bidhaa nje kimeongezeka


Sijui watanzania mnafikiria vipi hapo, mimi nina imani mazingira ndio uhai!!
Na vipi kuhusu suala la bidhaa watu, maana wataalamu wa Tanzania wamejaa nje ilhali nyumbani wamepaacha hoi!

1 comment:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kwakweli tumeharibu mazingira vya kutosha. mito na vijito vimekauka ile mbaaaaya. na tunaendelea kuuza misitu na kukata miti utadhani sio yetu.

mimi na wenzangu kadhaa tuna mpango kamambe wa kuhakikisha kanda ya ziwa inakuwa situ likuuubwa sana ifikapo 2015. labda itasaidia.

pia ni habari njema kwani sasa napanga kufanya kilimo kando kando ya mpaka wa tanzania na Rwanda, ie Karagwe