Jumamosi asubuhi nilikuwa nasikiliza BBC idhaa ya kiswahili, kwa wale wanaopenda kusikiliza kipindi hicho nafikiri na wao walipata mshangao kama mimi kwa taarifa ya utafiti wa Kodak.
Ati wanadai wanaume katika maisha yao hutumia takribani mwaka mmoja kwa kuwakodolea macho akina mama (wastani hutumia masaa 11 kwa mwaka), na sehemu kubwa ambayo hutumia kuwaangalia akina dada ni kwenye maduka makubwa aina ya supermarket. Tofauti na wanawake ambao hutumia takribani masaa 6 tu kwa mwaka kuwakodolea macho wanaume, na sehemu kubwa ya kukodoa macho ni kwenye mahoteli na baa!!
Hii habari ilinikumbusha habari ya utafiti uliofanyika katika nchi zinazoendelea, ambapo mambo ni tofauti,kwani wanaume hukodoa macho zaidi mitaani na hasa kwa baadhi ya maumbo ya akina mama ambayo ni tofauti na yale ya visura (mamiss). Na kulikuwa na tofauti ya ukodoaji kati ya wasomi na wale wenye kipato cha juu ukilinganisha na wale wa kipato cha wastani na chini. Sipendi kwenda kwa undani maana ninaweza kukiuka matarajio ya wasomaji......
Siku nyingine tukutane katika ukodoaji katika kioo
5 comments:
Mh, nilipomaliza kusoma post hii nimejaribu kujitafiti mwenye kama ni kweli huwa nakodoa. Lakini majibu si lazima kuyatoa kaka Chib ntafulia mahali.
Du, hata mie sikuwa najua, ila nimetafakari kwangu naogopa hata kuandika, maana nimejishangaa kwani hukodoa haswa, namuunga mkono Chib kwa kutokumwaga hadharani watu wasijebaki hoi!
chib wewe uliyeko rwanda kwa midada mizuuuri huwa inakuwaje?
Kamala , navaa miwani ya mbao na kuweka picha ya waifu :-)
Fadhy na Anony, .... DUH, sitaki kufikiri kwa niaba yenu...
Ya kweli hayo kaka Chib?
Post a Comment