Member of EVRS

Monday, 3 August 2009

Tabia ya Mtu Hufunzwa Toka Utotoni


Wiki iliyopita nilikuwa nasoma blogu ya MAISHA ambapo mwanablogu alikuwa anazungumzia kuadhibu watoto na kuwatukana kwa baadhi ya vitendo wanavyofanya ambavyo vingi huwa wanaiga kutoka kwa wazazi wao.
Mimi nakubaliana naye ya kuwa watoto wengi huiga matukio wanayoyaona kutoka kwa watu walio karibu nao, wazazi wakiwa sehemu kubwa ya msingi wa tabia za watoto.
Kama mzazi unatembea bararabarani ukiwa mchafu, au nguo dizaini, si ajabu mtoto wako akawa vivyo hivyo, ukimtukana ya kuwa yeye ni mchafu, mimi nafikiri utakuwa unajitukana mwenyewe!

5 comments:

jaz said...

hi chib...good to hear that it is good news for why you have been busy!!!! good luck with the exams and i will continue to check in!!! joyce

Fadhy Mtanga said...

Kaka Chib wahenga walinena, "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo."

Wazazi wengi huyafanya mambo mabaya, mathalani kutukana ama kuwa na mkono wa birika wakisahau kuwa watoto nao huiga.

Anonymous said...

Hiyo picha ni mfano, kama mtoto anatembea mtaani na ch.., na mama naye sijui ni bichikoma au nyanya puzo, akikua utamweleza nini

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wamependeza kweli kwali hawa. ni mtizamo

Yasinta Ngonyani said...

Nimekumbuka kitu ambacho wazazi wengi hujisahau au wanafanya makusudi kuongea mambo kuhusu majirani kwa mfano mama fulani yule ana makalio makubwa. Na kesho yake mtoto anaondoka na kwenda kucheza kwa majirani wale na bila aibu anasema au anauliza kwa nini wewe una makalio makubwa?