Member of EVRS

Tuesday, 25 August 2009

Umoja wa Watanzania Wanaoishi Rwanda Kuzinduliwa


Wasomaji wote na wapenzi wa blogu popote


Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda utazindua rasmi Umoja wa Watanzania wanaoishi nchini Rwanda mnamo siku ya jumamosi tarehe 29.08.2009 kuanzia saa 9.00 alasiri hadi saa 11.00 jioni. Shughuli hii itafanyika katika ofisi za ubalozi wa Tanzania hapa Rwanda zilizopo eneo la Nyarutarama, Jijini Kigali.


Watanzania wote wanaoishi Rwanda wanaalikwa kufika ili kuweza kuweka mshikamano mkuu.

Kwa watakaotaka ufafanuzi, wanaweza kupiga simu namba (+250) 252505400


Wote mnakaribishwa.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana! Nawatakieni kila la kheri nadhi ntashindwa kuhudhuria, lakini natamani ,,,,lol

Ugokko said...

Sio kawaida kwa ofisi za balozi kuandaa shughuli ya umoja kwa watanzania, kuna nyingine huwa na matusi kabisa iwapo utaenda kujitambulisha tu. Hii ya Rwanda ni ya mfano wa aina yake. Ningependa kumjua kwa jina balozi wetu huko.