Member of EVRS

Tuesday, 4 August 2009

Obama: The Servant of his People

Pale Rais anapowakaribisha na kuwahudumia wageni wake ikulu.
Nafikiri viongozi wengi wa Afrika na kwingineko hawawezi kudiriki kufanya hivyo.
Kwa mtazamo wangu nafikiri Obama alikuwa ana hamu ya kula nyama choma, ambapo wakenya ni maarufu sana duniani kwa nyama choma, na sharti la kula nyama choma ni lazima muwe wengi, hivyo Obama alitaka kukumbukia nyumbani Kenya.
Shukrani kwa mdau aliyenitumia hizi picha

9 comments:

Thom said...

Many leaders they do the opposite, they make people their servants!

Fadhy Mtanga said...

Mdau Thom kamaliza kila kitu. Afrika, wafanye hivyo wakati siku zote utawaona ndani ya suti?

Anonymous said...

Hata kama wanaenda kukagua kilimo cha mpunga na suti!

Mzee wa Changamoto said...

And who's the people?
Unajua mimi dhana nzima ya siasa yanichanganya. Wanang'ang'ania kuwa wapo walipo kwa sababu ya wananchi lakini sijawahi kuliona hilo. Wanasema Demokrasia ni pale Rais anapochaguliwa na wananchi wengi nchini japo ukweli ni kuwa anachaguliwa na wengi wa waliopiga kura. Mfano uwe na watu 100 waliojiandikisha kupiga kura ama wenye vigezo vya kupiga kura. Na siku ya uchaguzi, watu 65 waende kupiga kura na kati ya hao 65, 35 wamchague Rais. Ataonekana ameshinda kwa kura nyingi japo yawezekana wale 35 wote hawakupiga kura kwa kuwa hawamtaki mgombea na walijua atashinda. Ina maana majority (kura 65 hazimkubali).
Hapa Marekani ndio usiseme. Wanwaambia watoto kuwa wakiwa na umri wa chini ya miaka 21 hawawezi kuwa na maamuzi mema hivyo wasinywe pombe, ila akiwa na miaka 19 wanampeleka vitani huko akaamue kufyatua ama kutofyatua risasi. Amaaaaaaaaaa!!!
Paia kuna siasa za kuruhusu ama kukataza utoaji mimba. BIG ISSUE hapa nchini. Kuna wanaojionesha kuwa wanawajali wananchi wao na wanataka kuwapa UHURU wa utoaji mimba huo. Lakinikila anayetetea utoajia mimba hakutolewa na yuko hai. Nadhani tukiwaambia kuwa kwa kila mimba inayotolewa iendane na kuuawa kwa mmoja wa wanao-support hilo tunaweza kuona ni wangapi watajiandikisha ku-support utoaji mimba. Tuachane na hao, wale wanaopinga utoaji mimba hawana tatizo na vita. Kwa maana nyingine wanakwambia mzae mwanao, mtunze vema awe na afya na akitrimiza 19 tunaweza kumpeleka vitani aue ama auawe. Mmhhhhhhhhhhhhhh.
Sasa kwingine wanakwambia kiongozi fulani si mwanademokrasia kwa kuwa anaua watu wake, kwa hiyo watakachofanya ni kumuingilia kinguvu, kuua watu wake na pengine yeye, kisha kumuweka mtu wao, wampe vitu vya kuhonga na kujiandaa kwa uchaguzi kisha waitishe uchaguzi watakaosimamia wao halafu waseme sasa "tumeanzisha Demokrasia" Mmhhhhh.
Ndio maana hata hapa nauliza kuwa kiongozi huyu nimpendae anawahudumia watu, KINA NANIIIII????
Naacha nisije kuonekana MTUKUTU

Yasinta Ngonyani said...

Waliotangulia wamesema yote. Ila nami nasema tu nimefurahi sana na hivyo ndivyo inavyotakiwa kwani kusaidiana ni jambo zuri. Safi sana Obama

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sio lazima kumuiga Obama kwani hata kuvaa suti tulianza kwa kuwaiga wazungu wa ulaya

chib said...

:-)

Halil Mnzava said...

haya bwana!ila viongozi wetu bado wanasafari ndefu kufanya haya maana yale ya msingi tu kwa wananchi bado hayajafanyika!

SIMON KITURURU said...

Rais Kikwete afanye hivi ajidharaulishe!:-)