Member of EVRS

Wednesday, 26 August 2009

Josef Stallin: Dikteta Ambaye Anaanza Kukumbukwa
Stallin: Picha ya chini

Josef Stallin, aliyekuwa mzaliwa wa Georgia, ambaye alikuwa rais wa pili wa iliyokuwa Shirikisho la nchi za Kirusi, na ambaye inasemakana utawala wake ulihusishwa na mauaji ya mamilioni ya warusi wakiwemo waliokuwa wanaishi jimbo la Georgia wakati huo, ameanza kukumbukwa na baadhi ya wananchi wa Georgia na urusi kwa kile wanachosema wamechoka na utawala wa sasa ambao rais aliyepo madarakani anaendeshwa kama kikaragosi na waziri wake mkuu.
Waziri mkuu wa sasa wa Urusi, Putin, ndiye aliyemtangulia rais wa sasa bwana Medvedev, na wamekuwa wakilaumiwa kufanya vita iliyosababisha mauaji huko Georgia, na hakuna anayewachukulia hatua au kuwakemea.
Kwa mtazamo wangu:
Inapotokea wananchi wakatamani dikteta aliyekwisha kufa arudi na kuonekana ni bora kuliko wewe uliyepo madarakani, yapaswa ujiulize mara mbili mbili.
Hii ni changamoto kwa viongozi wetu hususan katika bara la Afrika.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mmmmmmhhh!!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kuna ppropaganda hapo kati ya mgharibi na mashariki.

SIMON KITURURU said...

Eti si ni kweli Rais Mkapa ndio nasikia anatarajiwa kuwa waziri mkuu katika serikali ijayo?:-)


Ila kuna jamaa alinitumia atiko moja la kiongozi wa Singapore katika kunishawishi kuwa kuna madikteta ambao ni bomba kwa nchi zao mpaka nikataka kutamani TZ angepatikana mmoja.

Unaambiwa jamaa aligeuza Singapore mpaka waliomchukia baada ya miaka michache wakawa ndio washabiki. Na aligeuza kuanzia maofisini mpaka nyumbani kwa watu.

Kwa kifupi ukitaka kujua alivyokuwa mtemi, alisababisha uwe msafi nyumbani kwako bila kuja kukukagua na Mtaani hata kitu kama lawalawa nyama a.k.a Big G ukitafuna na kukosea jalala kasheshe utaipata!Na hapo naongelea tu alivyogeuza nchi iliyokuwa chafu kuwa safi overnight.

Kwa ujumla ingawa ni kwa kitemi ila wanakuwambia Singapore isingekuwa ilivyo bila utemi wengi waijuavyo wanadai.

Bongo bado tunaongea ,kutenda bado twadai tunaumwa mgongo au kiuno wakati huohuo twazidi kuongea na kuremba misemo!:-(

Kuhusu Putin sina lakusema ila ananiua tu kwa jinsi sikuhizi anavyojiuza kwa wananchi kama sex symbol.Na sitashangaa ukisikia kawa Rais tena kwa kubadili katiba.

DUh!