Member of EVRS

Monday 10 August 2009

Ugenini: Pale chakula kikuu kinapobadilika

Mdau maarufu wa blog hii ambaye kwa sasa yupo Korea kusini, Emmanuel mwenye T-shirt ya njano alinitumia ujumbe ya kuwa anapitia wakati mgumu kwenye masuala ya misosi maana menu huko ni vyura, konokono, nyoka nk
Ukizingatia anatoka jamii ya wafugaji, na masuala ya nyamachoma nk ndio sebule yake, amelazimika kuwa mtu wa mbogamboga ila sijui..... kama kweli ana uzalendo....

Mdau, ninakutakia masomo mema huko Korea.

Picha: Kwa hisani ya Emmanuel akiwa Korea ya Kusini

5 comments:

Thom said...

:-o

Yasinta Ngonyani said...

Ohhh! pole sana maana chakula ni muhimu sana katika maisha ya binadamu. Kula chura, mmmh kazi kwelikweli basi kula hizo mbogamboga je? atakuwa huko kwa muda gani?

Fadhy Mtanga said...

Piga menu mwanangu, mböna wao wala then hawafi.

Pole sana.

George, Uk. said...

hao viumbe wakipikwa na kutiwa viungo na kapilipili kwa mbali,usipoangalia waweza kujiuma ulimi wakati wa mlo.
Duh ila yaitaji moyo... inabidi wakati wala,unaweka picha ya kuku alokaangwa vilivyo mbele ya upeo wa mcho yako.
any way cha msingi protini ya nguvu waipata.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

tafadhali msile wanyama wala wadudu. mimi nawashangaa hata wale mnaokula ng'ombe, mbuzi nk. ujasiri kama wenu huo ndio unaowafanyha wakolea wale hivyo viwashangazavyo. SHINDWA