Member of EVRS

Thursday 11 March 2010

Tajiri Mpya wa Mwaka 2010 Duniani

Carlos Slim Helu (Pichani) raia wa Mexico ndiye mtu tajiri kuliko wote duniani kwa mwaka 2010 kutokana na matokeo ya matandao wa Forbes.
Helu ambaye anaendesha biashara ya mambo ya mawasiliano ikiwamo na simu amewapiku raia wa Marekani Bill Gates and Warren Buffett ambao wamekuwa wanatawala nafasi mbili za juu, na Bill Gates kuzidiwa kwa mara ya pili katika miaka 14 iliyopita.

Utajiri wa Helu unakaribia kufikia kiwango cha dola za kimarekani bilioni 53.5 akiwa amemwacha Bill Gates katika nafasi ya 2 ambapo utajiri wake unafikia kiasi cha dola bilioni 53 na Buffet akiwa wa tatu.
Nafasi ya 4 na 5 zinashkiliwa na mabilionea wa India.

Utajiri wa Helu unakadiriwa kuongezeka kwa kiasi cha dola bilioni 18.5 kwa miezi 12 tu iliyopita.

Kwa ujumla Marekani bado inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya mabilionea duniani, ingawa China imekuwa inakuja juu

Wale Mafisadi wetu wasitarajie kwa wizi wao huo wataweza kuingia kwenye chart kama hizi!

Source: Forbes.com au hapa

4 comments:

Fadhy Mtanga said...

Kaka Chib hao jamaa ni kiboko.
Hawa mafisadi wetu nao ni matajiri sana ila sema tu kwa vile biashara zao siyo halali ndo maana hawavumi.

Simon Kitururu said...

Jamaa bonge la TAJIRI ila kunatetesi ni bonge la bahiri.

Watu na pesa wanachekesha. Unaweza kukuta masikini anatumia pesa kuliko TAJIRI.:-(

Yasinta Ngonyani said...

Hongera na yeye mimi sitaki kuwa tajiri.

chib said...

@ Simon, :-)
@Fadhy, tofauti ya vitajiri vyetu ni kweli ni vijizi tu na kuuza madawa ya kulevya, tofauti na wenzetu wana biashara halali hata kama wanaiba kwa kuweka gharama za juu kununua mali zao, lakini unalipa mwenyewe kwa uwazi tofauti na akina Richmond wetu