Member of EVRS

Sunday, 14 March 2010

Polisi Tanzania na Harakati za Kutokomeza Rushwa

Jeshi la polisi Tanzania limeweka mkakati wa kupunguza rushwa, (nasisitiza kupunguza, na sio kumaliza) katika jeshi hilo kwa kuwazawadia polisi watakaokataa kupokea rushwa na kuwafikisha watuhumiwa katika mikono ya sheria.

Zawadi wanayopewa ni sawa na kiasi walichokataa kupokea kutoka kwa mtuhumiwa.
Wikii hii tumeshuhudia askari mmoja akiwa hundi ya mfano (dummy cheque) ya kiasi cha Sh milioni 4 baada ya kukataa rushwa ya kiasi cha dola za kimarekani 3,000.
Hii inatiamoyo kwa kujenga jeshi dhubuti lenye nidhamu na uaminifu.

Pia mwezi huu tumeshuhudia watu wakikamatwa na madawa ya kulevya huko Tanga, tulimshuhudia kamanda mmoja akisema hawatajali wenye biashara hiyo ya madawa ya kulevya ni vigogo au watu wadogo, sheria ni msumeno na watashughulikiwa wote.
Pia raia mmoja wa Kenya na Mwingine wa Ujerumani walikamatwa na kiasi kikubwa cha fedha bandia za kitanzania na pia yuro na dola nyingi tu.

Bado ninajiuliza, je ni kweli jeshi la polisi limebadilika kikweli au ndio tumekaribia uchaguzi basi kila mtu anajifanya kuanza kuwajibika!!
Kwani imekuwa ni kitu cha kawaida kupeleka kesi polisi, na unaishiwa kuombwa chochote ili uwawezeshe polisi kufanya kazi yao

Siku za nyuma tulishuhudia mkuu fulani wa polisi akisema wamepokea orodha ya watu wanaojishughulisha na madawa ya kulevya, na akasema kwenye vyombo vya habari ya kuwa orodha hiyo inatisha, maana majina ya wahusika inaonekana yalikuwa ni ya watu mashuhuri, sifahamu hiyo orodha ilifika wapi maana wenye nchi walikataa kabisa kuiweka hadharani orodha hiyo kwa wananchi ili nao wawafahamu watu wanaoangamiza vijana kwa biashara yao hiyo.
Kwa sasa imekuwa kimya kabisa.

Swali kero:
Tunawazawadia polisi, ni sawa, lakini je watuhumiwa na wao watahukumiwa kihalali? Je, na wanaowatuma kuleta madawa hayo nao watashughulikiwa?
Suala la polisi kuomba rushwa, nalo limewekewa mikakati gani?

Watanzania sasa tumechoka na mikakati ya kulindana

3 comments:

Upepo Mwanana said...

Nafikiri jeshi limeamka sasa.
Tuwaombee kila heri watokomeze rushwa

chib said...

Mwanana, mie naona bado kabisa

SIMON KITURURU said...

Harakati hizi za kutokomeza rushwa hazina Danganya toto kweli ukizingalia UMASIKINI uliovyoshamiri?