Member of EVRS

Tuesday 2 March 2010

Ajali ya Ndege ya Air Tanzania Mwanza

Ndege ya shirika la ndege la Tanzania Boeing 737 - 200 yenye namba ya usajili 5H - MVZ jumatatu tarere 1 machi 2010 asubuhi imepata ajali wakati ikitua kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza.

Baada ya kutua ilikwenda umbali wa kama mita karibu 800 kabla ya kuacha njia na kuingia kwenye nyasi na kusababisha tairi la mbele kurudi ndani na hivyo sehemu ya mbele ya ndege hiyo kugusa ardhi na injini moja kuharibika.

Hakuna abiria aliyejeruhiwa, ingawa abiria walilazimika kukaa kama dakika 20 ndani ya ndege baada ya kusimama wakisubiri ngazi iletwe ya kushuka!

Kulikuwa hakuna upepo mkali uwanjani, isipokuwa kulikuwa na ukungu kiasi na mvua iliyokuwa imenyesha ilisababisha sehemu ya kutua na kurukia ndege kuwa na kabwawa ka muda. Hali hii ndio inasemekana huenda ndio ilisababisha ajali hiyo.

Kama ni kweli, inaweza kushangaza kwani miaka ya nyuma kama sijasahau sana, ndege ya shirika hilo hilo iliwahi kukwama tena baada ya kutua kwa sababu ya uwanja kujaa maji.
Kama hali hii haijarekebishwa, hapo ni kutia maisha ya watu rehani!
Sasa huyu ng'ombe wa maskini vipi jamani!

4 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ng'ombe wa masikini hazai. Sijui kama ni ajali haina kinga au ni vinginevyo. Cha muhimu ni kwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha. Hilo ni shirika linaloendeshwa kwa pesa za umma kwa hivyo hakuna neno watanunua nyingine!

Fadhy Mtanga said...

Pole zangu ziwe kwa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo. Najaribu kukisia walikuwa katika hali gani. Shukrani zetu ni kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwanusuru.

Yasinta Ngonyani said...

Nami nasema namshukuru Mwenyezi Mungu kuwa hakuna aliyepoteza maisha. Kama ndege tutatengeneza au nunua nyingine lakini roho za binadamu ni ngumu kuzipata tena.Amina

Edet Onen said...

Thanks for visiting my blog, I appreciate. . .
Keep up the good work.