Member of EVRS

Monday, 22 March 2010

Kwa Kenya: Ni Mzaha Tu

Baada ya Kenya kutangaza rasmi sheria ya kuzuia kuvuta sigara hadharani. Halmashauri za miji ziliambiwa kutoa matangazo kwa wananchi kuhusiana na sheria hiyo mpya ili wananchi wazifahamu, kwani kuivunja kutapelekea kushtakiwa mahakamani.

Kila mji uliandika matangangazo kama ifuatavyo:

Mombasa
Uvutaji wa sigara umepigwa marufuku kuanzia leo.Watakaopatikana wakikiuka amri hii wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Nyote zingatieni.

Kiambu:
Wanyuanji wa thigara washunge sana . Unyuanji wa thigara bere ya watu hata huko ije umefigwa marufuku na kaju kuanjia reo.

Machakos:Wavulutanji tusikala wasunge sana . Sasa kuvuluta tusikala ni maluvuku na kanzu ya Masaku itawasukulia atua kuvwa sana.

Kisumu:Atenson Plis!!! Mifuto sgara adharani sasa omepigwa marofuku. Okipaatwa, ibiro yie Kodiaga! Apana furuta Plis!!

Wajir:
Habana iko buruta sigara. Yeye lishapigwa marufuk na sisi tagaamata mutu bahala yaghe kiburuta.

Kericho:
Gutoga leo gugunywa na gufuruta sigara sisi nagshagataasa. Haguna!! Charipu wee taona!!!

Kisii and Nyamira:
Akuna kukunywa sigara hapa ndani na inche kuansia reo. Mutakaobatikana mutakura kiboko saa hiyo hiyo. Wote munaombua kujiatari sana.

Kakamega:
Hakuneko kufuruteko sikara hapa ntani kudoka leo. Ukipatikaneko ukifurutako sikara udafundishekwho atapu kali na utaoneko djamdemaguni!

Miji mingine watendaji walikuwa wameenda kwenye kozi ya kiswahili, kwani matangazo ya awali yaliandikwa kwa lugha za wenyeji, hivyo yakashindwa kuhakikiwa na mabaraza ya miji hiyo, na kwa hasira wakawaambia waende kujifunza kiswahili!:-(

Namshukuru Mdau kwa kunipatia habari hii.

6 comments:

Anonymous said...

Ha haa haa, siku nyingine tuletee utani hu siku ya ijumaa itatusaidia kuondoa uchovu wa wiki nzima, ha ha haaa

Fadhy Mtanga said...

Ha haaaa haaa haaaa haaaaaaa!
Saa ingine hii omenifanya kuchekereka muno.

Kaka Chib we mkali. Nimecheka hadi machozi.

Ahsante sana, you have made my day.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kwikwi kwi kwikwi kwi kwi

tehehehehehetehetehhhhheeeee

puuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!! HARUFU KALI

Anonymous said...

@Kamala, umenifanya nicheke zaidi ha ha haaa

chib said...

Wengine hapa hamjatulia :-(

SIMON KITURURU said...

:-)