Member of EVRS

Monday, 8 March 2010

Ujumbe Wangu kwa Siku ya Wanawake Duniani

Leo ni siku ya WANAWAKE duniani.

Hakika ni siku kubwa labda pengine kuliko zote.
Kuna watu waliwafananisha wanawake na maua yanayodumu, kwani kila mtu anapotaka kupumzisha akili yake, basi anapokaa katika bustani iliyo na maua hujisikia furaha moyoni. Ni kweli pia katika dunia yetu, watu ambao wanaleta furaha ya kweli, upendo na amani ni wanawake.


Hata kwa wanaume makatili na wanaopigana vita na kuishi mafichoni, sehemu pekee anaposema anastarehe ni pale anapokuwa na mwanamke (Ingawa mara nyingi kwa hapa ni ukatili na ubabe).

Kwa mantiki hii, kuna baadhi ya watu wameshindwa kuelewa umuhimu wa wanawake katika maisha yetu ya kila siku. Sitaweza kuwasemea sana wanawake, lakini nafikiri kwa upande wao starehe yao kubwa ni pale panapokuwa na amani na upendo. Labda mwanaume ni sehemu tu ya starehe (Naomba msininukuu hapa).

Ujumbe wa mwaka huu unazungumzia fursa sawa na maendeleo kwa wote. Tunapaswa kuuenzi ujumbe huu kwa vitendo.

Napenda kuwashukuru na kuwapongeza wanawake wote Duniani. Sitaki kuwa mchoyo wa fadhila, kwani shukrani zangu za kipekee nampa Mama yangu mzazi kwa kunilea na kunikuza mpaka leo nilipofikia hapa. Pia shukrani nyingine ni kwa mke wangu ambaye muda wote yupo nami hata kama umbali unatutenganisha kwa nyakati fulani, pia binti yangu ambaye ana mapenzi makubwa kwetu wazazi (unconditional love), ambaye amekuwa chachu ya furaha katika maisha yetu ya kila siku.
Nawashukuru na dada zangu na bila kuwasahau marafiki zangu wote wa kike ambao wamekuwa wakinitembelea hapa kwenye kibaraza na kutoa michango mbalimbali ya mawazo ingawa hatujawahi kuonana maishani zaidi ya kukutana kwenye mitandao hii ya kuandika na kufyatua.

Najivunia kuwafahamu Wanawake, najisikia furaha kuwapa heri katika siku yao, na najisikia ya kuwa wanahitaji msaada wetu sisi wanaume ili waweze kujikomboa kimaisha.

God Bless All Women

7 comments:

Mija Shija Sayi said...

Asante sana Kaka Chib, mbarikiwe pia nyie wanaume kwa vile mmekuwa kiungo kikubwa katika furaha ya wanawake, tunaomba Mungu awabadilishe wale wachache ambao bado hawajaona umuhimu wa mwanamke, hali kadhalika wanawake walalamishi wanaodhani wanaonewa masaa yote.

Polepole tutafika.

Ameni.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kaka Chib. Ujumbe mzuri kweli nimesoma na mwisho nikajikuta kwa duraha nalia. Upendo Daima.

Faustine said...

....Bw. Mkubwa ujumbe wako ni maridhawa.....

Upepo Mwanana said...

Tunashukuru sana kwa kutukumbuka.
Be our part as we are part of you.
We need your support.
God bless you too

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ukijiuliza mengi juu ya wanaweke duhu, labda heri yao.

lakini kama ningekuwa mlristo ningesema hivi;

"alaaniwe Eve / hawa Kwa kudanganyika na kula tunda la mauti limletealo chib kifo na mauti AMina"

hivi hii siku ya wanawake nani aliiteua ni mwanamke au ndo ile alipokula tunda na kumpa dear wake?

Wife said...

Asante mume wangu. Mungu akubariki nawe pia.

mumyhery said...

Shukran