Member of EVRS

Tuesday, 16 March 2010

Sindano Iliyomuua Michael Jackson Kupigwa Mnada?


Kumekuwa na habari za udaku ya kuwa ile sindano na bomba lake iliyotumika kumchoma na kusababisha kifo cha Michael Jackson kuna mjanja anataka kuipiga mnada na kuiuza kwa kiasi cha pauni milioni 5 za uingereza amabazo ni karibu sawa na madafu ya kitanzania (shilingi) zaidi ya bilioni 12.

Wazo hilo lilikuja kwa mnazi huyo baada ya mahakama kusema hailihitaji tena bomba hilo la sindano kwa sasa kwenye ushahidi wa kesi ya aliyekuwa daktari wake Murray ambayeamefunguliwa kesi ya kumuua MJ bila kukusudia kwa kumchoma sindano inayotumika kulaza wagonjwa kwenye chumba cha upasuaji.

Thamani halisi ya sindano na bomba lake haizidi madafu 500.

Habari hizi zimeishtua sana familia ya Michael Jackson na wamekasirika sana, na wanafanya kila juhudi kuzuia uhalifu wa namna hiyo.

Lakini mjanja huyo naye ni mwerevu, ameshapata jopo la mawakili kumuongoza mpaka apate uhalali wa kisheria kuuza hilo bomba, na tayari amesha zunguka kwenye minada maarufu huko Las Vegas kutafuta soko.


Kwa kimombo bofya hapa

6 comments:

SIMON KITURURU said...

Ama kweli duniani kuna mambo kwa kuwa tutasikia hiyo ni moja ya ujasiliamali mwanana pia.

Yasinta Ngonyani said...

Sasa kweli dunia imekwisha ni mwisho wa dunia mnada mpaka sindano! Duh Sijui huko tunakoenda itakuwaje!!

chib said...

Kufa kufaana. Dunia hii, kweli ni tambara bovu.
@ Kitururu.. Ujasiliamali Mwanana :-)

Laura said...

Don't worry about the T-Shirt, are just the lyrics of a song (Kill All Your Friends by My Chemical Romance). I needed it -I mean, a T-Shirt with this kind of lyrics- for a coreography for P.E. at school.

John Mwaipopo said...

hata bure siitaki. like you guys have said, dunia ilijiishia kitambo. hii tuliyomo ni mabaki yake na mfano wake. a syringe!

John Mwaipopo said...

hata bure siitaki. like you guys have said, dunia ilijiishia kitambo. hii tuliyomo ni mabaki yake na mfano wake. a syringe!