Member of EVRS

Sunday 28 March 2010

Ni sahihi au Si sahihi?


Katika pita pita yangu katikati ya mji wa Kigali... Nilimkuta mama huyu katika kituo cha mafuta akiwa na juhudi kubwa ya kumwagilia lami mpya ambayo ndio kwanza imewekwa siku iliyopita.
Jua lilikuwa ni kali na mara kadhaa alikuwa anakunywa maji hayo kutoka kwenye mpira wa kumwagilia ninafikiri ili apoze kiu.
Hakukukuwa na vumbi wala uchafu kwenye hiyo lami, yaani ilikuwa bado ni mpya.
Mimi sio mkondarasi wala sina ujuzi wa uhandisi, lakini sijawahi kuona lami ikimwagiliwa maji baada ya kuwekwa. Nimewahi kuona wanamwagilia maji kabla ya kuweka lami nafikiri ni kwa ajili ya kushindilia vizuri kifusi kinachowekwa nk.
Kutembea ni kujifunza mengi, kwa hili sijui kama nimejifunza au nimepotoshwa :-(
Nawatakia mapumziko mema ya wikiendi.

5 comments:

Anonymous said...

One can only hope that there will be enough water left throughout the summer months...

A nice Sunday for you.

Fadhy Mtanga said...

Duh! Jamani kitu kipya si kinasafishwa kwa ussongo ili kizidi ng'aa?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

usilolijua litakusumbua.

harafu umesema, nanukuu, """Mimi sio mkondarasi wala sina ujuzi wa uhandisi, lakini sijawahi kuona lami ikimwagiliwa maji baada ya kuwekwa""""""
mwisho wa kunukuu

kama hujawahi ona sasa nani anatuadithia hii?? umewahi ona na ndio maana unasimulia vinginevyo unatudangya eti ulimwona aki... wakati hujawahi ona!

mumyhery said...

na kweli Kamala jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza

Anonymous said...

;-)