Member of EVRS

Wednesday 10 March 2010

Arsenal 5, FC Porto 0

Timu ya Arsenal, pamoja na kuwa na majeruhi wengi tena wachezaji wa kutegemewa imeonyesha kuwa vijana wake yoso ni moto wa kuotea mbali baada ya kuifumua FC Porto ya Ureno kwa mabao 5 - 0.

Mchezo ulichezwa uwanja wa Arsenal - Emirates na kuhudhuriwa na washabiki waliojaa uwanjani mpaka pomoni.

Najaribu kutafakari kama ndio ungekuwa mpira wa kwetu wa Simba au Yanga kukatokea timu ikashindiliwa mabao yote hayo, nahisi viongozi wa timu wangeishakuwa katika mkao wa kusubiri kupinduliwa uongozini na kusingiziwa wamekula mlungula.

Na Sangoma angekuwa ameshajichunia mapema, maana kuna baadhi ya wachezaji bila kupiga ramli na kuomba matokeo ya giza, basi siku hiyo hawawezi kucheza :-(
Sikushangaa wakati kocha mmoja mzungu alipolalamika kuwa tatizo kubwa la timu za Bongo wanaamini sana majuju kuliko kucheza mpira.

Mie ninashauri wakaguzi wa timu kabla ya pambano wawapige sachi wachezaji kujua kama wamebeba transistor ama la, maana hizi zinawaharibia saikolojia na ari ya kutafuta ushindi :-(


Congrats Arsenal!!!

1 comment:

ahmed said...

I visited to this sied and i got a information that another sied visited before a month
Work from home