Member of EVRS

Sunday 6 March 2011

Mkutano wa Mwaka wa Umoja wa Watanzania Waishio Rwanda - UTARWA

Jana Jumamosi Umoja wa watanzania waishio Rwanda walifanya mkutano wa mwaka katiaka hoteli ya Foeyes ambayo inamilikiwa na watnzania hapa mjini Kigali, Rwanda.
Mkutano huo ulikuwa ni wa kujadili mambo mbalimbali yaliyotukia katika umoja huu kwa mwaka mmoja uliopita ambao ulikuwa wa mafanikio sana.

Mbali ya hayo, pia ulipokea taarifa kutoka ofisi ya ubalozi wa Tanzania hapa Rwanda kuhusu matukio mbalimbali yaliyotokea nyumbani Tanzania tangu mkutano wa mwisho uliofanyika mwaka jana. Miongoni mwa taarifa zilizopokelewa ni pamoja na milipuko ya mabomu huko Gongo la Mboto na hali ya tatizo la umeme nyumbani na hatua zinazoendelea kuchukuliwa.

Mbali ya mkutano huu, kulikuwa na chakula maalumu cha kitanzania kiliandaliwa kikisindikizwa na muziki wa kitanzania pia. Vyote vilifanywa kama kuukaribishwa mwaka mpya wa 2011.

Pata habari picha hapa chini:

Wajumbe wakiingia kwenye chumba cha mkutano

Ukumbi wa Mikutano hapa Kigali, Rwanda ulifanyika katika mgahawa wa Kilimanjaro ndani ya Foeyes Premier Hotel

Maandalizi ya mwisho kutoka kwa viongozi wa UTARWA

Wajumbe wakipitia dondoo kabla ya mkutano kuanza


Mkutano ukiendelea chini ya Uongozi wa mwenyekiti Josphine M- Ulimwengu kabla hajang'atuka rasmi huku akiwa na mgeni mashuhuri mhesh Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Dk Matiko aliyekaa katikati



8 comments:

Upepo Mwanana said...

Kila la heri katika mwaka mwingine wa kazi

malkiory said...

Hongereni sana kwa umoja na mshikamo baina ya watanzania mliopo Rwanda. Rwanda ni mfano wa kuigwa na nchi zingine kutoka katika bara la Afrika kwa mikakati na sera zake nzuri za kimaendeleo tofauti kabisa na Tanzania.

Goodman Manyanya Phiri said...

Mimi ninao wasiwasi hamkula vyakula tuliyezowea sisi Tanzania. Kama ningepata uthibitisho, mbona ningemega sasa hivi ugali wangu hapahapa Pretoria nilipo na kumeza kwa mboga ya kimawazo tupu!


mmmmh... Labda mlikula siasa tu! Viva Tanzania! Viva Rwanda!

Simon Kitururu said...

Mmmmh!

Yasinta Ngonyani said...

Hongera kwa ushirikiano mlionao. Upendo daima

chib said...

Ha haa haa Goodman! Tulikula vyakula vya kitanzania vilivyopikwa na watanzania. Hat kwa wale wanywaji, walipata vileo vya kitanzania tu, kwani hakuna kilicholetwa kama hakikutengenezwa Tanzania.

Goodman Manyanya Phiri said...

Basi sikupotea katika ka Watanzania miaka 1985-1994 eti?

Karibuni sana nanyi kujifunza Kizulu http://ndimiafrika.blogspot.com/ (baadaye nitatoa hata mafunzo ya lugha ya Kikaburu---Afrikaans)

Kizulu na KiAfrikaans ndizo lugha mbili za kienyeji zilizovuma Afrika Kusini. Ukiongea moja yake, huwezi kabisa ukachomwa moto na wale wenye ugonjwa wa XENOPHOBIA!

chib said...

Itabidi kufanya mazoezi ya kuongea ukinatisha ulimi kwenye koo kabla hatujajifunza kizulu