Member of EVRS

Friday 11 March 2011

Japan Yakumbwa na Tsunami

Tetemeko kubwa la ardhi limetokea km 150 kutoka ufukwe wa Japan karibu na mjo wa Tokyo kama saa 3 zilizopita na kusababisha maafa makubwa.


Tetemeko hilo lilikuwa na nguvu za 8.9 katika vipimo vya tetemeko.

Pwani ya Japan ilipigwa na mawimbi yenye urefu wa mpaka mita 4 hadi 10 na kusababisha mafuriko katika jiji la Tokyo na miji mingine.

Mitaa imejaa maji nab ado yanaongezeka, mito inafurika, barabara na madaraja yanabomoka, na watu walio kwenye magari wanashuhudia maji yanawafuata kwa kasi na kuwazoa bila kujisaidia.

Kibaya zaidi, kituo cha kusafisha mafuta kimojawapo kimelipuka moto mkali sana ambao unaonekana kuvielemea vikosi vya kuzima moto.

Tahadhari imetolewa kwa watu wanaoishi karibu na Japan ikiwa ni pamoja na Sehemu ya Urusi, Indonesia, Philippines, Taiwan, Visiwa vya Marshal, Fiji, Guam, Papua New Guinea, Kiribati, Hawaii. Sehemu nyingine ni Australia, New Zealand, Amerika ya Kusini hasa Chile na Ecuador, pia hadi Mexico ya kuwa wajiandae na kuchukua tahadhari kwani kuna uwezekano maeneo hayo kufikiwa na Tsunami hii. Imekadiriwa ya kuwa kwa sasa hivi, mawimbi ya bahari kutokana na Tsunami yanasafiri kwa kasi kubwa.

Mpaka sasa huko Japan, kuna vifo kadhaa vimekwisha tokea na watu wengi hawajulikani mahali walipo.

Serikali ya Japan imewaomba wananchi waliopo eneo la janga, waelekee sehemu zenye usalama ambazo zipo kwenye miinuko au majengo marefu yaliyo imara.

8 comments:

malkiory said...

Mungu awafariji katika kipindi hiki kigumu cha maafa ya Tsunami. Hapa ndipo ukomo wa sayansi,maarifa na uwezo wa binadamu.Tupende tusipende lazima tuamini katika uwepo wa mungu.

emu-three said...

Hizo ni dalili za kuonyesha utukufu wake, kuwa kuna mambo tutajitahidi lakinimengine yanategemea utashi wake...Nakuunga mkono Mkuu Malkiory.
Wasiwasi wangu ni kuwa huyu jamaa SUNAMI akianza anakwenda mbali zaidi ya wanavyokadiria, sasa ni vyema huku kwetu tukajihami,...ufukweni huko muwe waangalifu

Simon Kitururu said...

Pole zao !

Tsunami zimeniondoa kabisa hamu ya kuwa na nyumba ufukweni, kwa maana TETEMEKO linabwenga Japani wewe umejilalia Hawaii uko swari tu ghafla Tsunami limekufuata mpaka huko.

Si inakumbukwa lile tetemeko jingine lililoikumba Thailand na nchi za maeneo yake mawimbi makubwa yalikuja mpaka East Afrika kwa waliojituliza tu ufukweni bila kujua kuna wimbi linawajia?

EDNA said...

Duuuh Mungu na awalinde,maana hii inatisha.

John Mwaipopo said...

Mungu ndiye mpangaji wa yote. Huumba na huumbua pia. Ukuu na utukufu wake utamalaki.

Mungu awajaalie rehema, neema na uvumilivu katika gharika hili.

@ simoni, kumbe dili ni kujisogeza milimani? lakini kule 'thame' hata milimani land slide zilitokea hivi karibuni.

Simon Kitururu said...

@Mkuu John: Halafu napafahamu kabisa pale mmomonyoko wa ardhi ulipotokea na nishawahi kupita maeneo hata kwa kutafuta denge ambayo ndio pombe ya kienyeji kule.:-(


Naona hapa duniani pakukimbilia siku yako ikifika hapapatikani.

Leo hii hii nnimesikia kuna mtu jumapili alifariki kwenye kanisa fulani kisa kapaliwa na mvinyo na kimkate cha chakula cha bwana!:-(


Ubinadamu nishai yani leo unaweza kuwa Charles Taylor Rais wa Liberia kesho Mfungwa kwa wadachi huku waafrika wenzako wakishangilia!:-(

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mungu Awalinde kuwafariji. Kama binadamu bado kuna mambo ambayo yako juu ya uwezo wetu wa kiakili, kiroho na kimwili...

Christian Bwaya said...

Inasikisha sana. Mwenyezi Mungu atunusuru.