Mwishoni mwa wiki iliyopita, Umoja wa Watanzania wanaoishi Rwanda - UTARWA - Ulifanya sherehe fupi ya kumuaga aliyekuwa mwenyekiti wa umoja huo Mama Josephine Marealle- Ulimwengu ambaye amepata kazi mpya ambayo inashughulikia masuala ya watoto kwa nchi sita zilizo katika ukanda wa Afrika ya Kati.
Ofisi yake itakuwa Addis Ababa, Ethiopia.
Kabla ya kupata kazi hiyo mpya, Josephine alikuwa mwakilishi mkazi wa shirika la CARE International kwa hapa Rwanda.
Katika mambo aliyowaasa watanzania wanaoishi Rwanda, aliwasihi kujituma, kufanya kazi kwa malengo ya kujiendeleza kitaaluma na kiutendaji na pia kusisitiza kukumbuka na kufanya shughuli za maendeleo nyumbani Tanzania.
Na mwisho alisisitiza, ya kuwa wasiwe waoga kufanya maamuzi ambayo wanahisi yatawaletea maendeleo kimaisha na kiutendaji.
Mwisho wa kauli mbali mbali za viongozi wa UTARWA akiwepo pia balozi wetu nchini Rwanda, Watanzania waliburudika kwa vyakula, vinywaji na muziki mwororo wa nyumbani ukichagizwa na utani wa makabila mbalimbali ya Tanzania.
Pata habari picha hapo chini!
Mwenyekiti Mpya wa UTARWA Bw,. Thambikeni akisoma risala kwa niaba ya wana-UTARWA |
Mlezi wa UTARWA Mhesh. Balozi wa Tanzania nchini Rwanda akitoa wosia |
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Mama Josephine Ulimwengu akipokea zawadi ya UTARWA kutoka kwa Balozi Dk Matiko |
Josephine akiifurahia kwa moyo wote zawadi aliyopewa |
Kauli ya kuwaasa wana UTARWA |
Wana UTARWA wanabadilishana hili na lile huku wakisubiri "Ndafu" |