Member of EVRS

Friday 22 January 2010

Tafakari ya Wikiendi



Wakati wa sikukuu za Krismas, mimi na familia yangu tulienda kupumzika Laki Kivu Serena Hotel. Nitatoa picha za mandhari nzuri ya huko baadaye.

Huwa mimi ni mpenzi wa kuangalia michoro au sanaa zozote kwa kuzitafakari.

Key holder hii ilinichukulia muda wangu kuitafakari, na niliweza kupata mapumziko ya fikara nyingine za kazi na uchovu kwa kukaa naitafakari hii sanamu ya huyu nyani wa milimani (mountain gorilla).

Nakupa nawe tafakari ya wikiendi.

7 comments:

Mija Shija Sayi said...

Huo msumari wa kuning'inizia funguo kwanini umegongewa kichwani na si sehemu nyingine ya mwili?
Hapo ni kwamba kichwa ndo ufunguo wa maisha yako.

Yasinta Ngonyani said...

Au pengine kuna aliyetaka kufungua na kuona kama nyani ana ubongo wa aina gani? AU labda inaonyesha kuwa huyu nyani hakuwa huru....ngoja kwanza nikune kichwa...mmhhh!!!

Juma4 said...

Sikuwa na wazo lolote, lakini kwa mawazo hayo hapo juu, ninamuona nyani yeye ametabasamu tu, tena kakaa kitako, sasa sijui anamfurahia mgeni au ana ashiria kuwa wanyama wana akili zaidi kuliko binadamu kwa sasa

John Mwaipopo said...

inaonyesha 'jasiri haachi asili' ikimaanisha binadamu eti tuliwaigi kuwa nyani. swali: mbona nyani wa siku hizi hawaelekei kuwa binadamu siku za mbele?

kazi ipo

chib said...

@ Mwaipopo.... :-)

Anonymous said...

Mimi naona huyo nyani kama kahifadhi au kaficha kitu fulani. Huo ni ujumbe tosha kwamba watu wajikinge na janga la ukimwi huko vyumbani!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

chumba chako kuna nyani hata kama humwoni!