Member of EVRS

Friday, 22 January 2010

Bujumbura at a Glance

Bujumbura, the capital city of Burundi, is rather small, cheaper and peaceful.
Ukiondoa Miji ya Tanzania na Mombasa, Bujumbura ni mji unaofuatia kwa kuongea kiswahili zaidi kuliko miji mingine mingi ya Afrika Mashariki.
Kiingereza ni nadra kukuta watu wakiongea, ila kifaransa kina mizizi zaidi, si ajabu kukutana na wafanyabiashara wanao ongea kiswahili, lakini pale unapotaka kulipa wakakutajia kiasi cha pesa za kulipa kwa kifaransa, wakishindwa kutamka kwa kiswahili hizo namba, na hasa wakijua umetoka Tz, inakuwa taabu, maana wamezoea namba zinazotamkwa ki-Congo, kama thelathini itatamkwa makumi tatu, sabini watasema makumi saba.

Mbali ya barabara za katikati ya mji kuwa safi, lakini hazina taa, utakuta milingoti ya taa imejaa, lakini yote haina taa kama baranara hii maarufu ya UPRONA ambako kuna ofisi kadhaa za ubalozi haina hata taa moja ya barabarani


Kuna majengo machache mapya, na mengine yanaendelea kujengwa.
Maisha ya Bujumbura ni nafuu kidogo ukilinganisha na Kigali - Rwanda. Kwa wastani gharama za maisha Bujumbura ni kama nusu hivi ya Kigali.
Hoteli nzuri zipo, lakini sio nyingi sana.
Niliyoipenda sana ni Lake Tanganyika Hotel (Hotel Club du Lac Tanganyika)


Ipo mwambao wa Ziwa Tanganyika, ina mandhari nzuri na pwani safi yenye mchanga mweupe. Milima ya Congo inaonekana kwa mbali kwenye ng'ambo ya pili.
Kama kawaida wapenzi wa samaki hapo tulifaidi hasa. Nilijipatia samak aitwaye Captain, sikuwahi kumuona kabla!
Ziwa Tanganyika ambalo sehemu kubwa lipo Tanzania, ni ziwa linalosifika kwa kuwa ni moja ya maziwa yenye kina kirefu duniani, pia ndio refu kuliko yote duniani likiwa na urefu wa karibu km 600, na pia linasemekana lina hifadhi maji kiasi cha wastani wa 15% (1/6)ya maji baridi (fresh water) yote duniani. Pia ndilo hasa chimbuko la mto Nile.
Pia niliduwaa kidogo kukuta matangazo ya vivutio vya Tanzania ambapo wanao utaratibu wa kuwaleta wageni kutembelea mbuga za wanyama na vivutio vingine vya Tanzania.
Wabongo mpoooo. Mpaka mtangaziwe eeeh!
Enjoy your weekend!!!



9 comments:

SIMON KITURURU said...

Hivi maisha ya Kigali ughali wake ni kama Dar?

Nahamu kweli ya kutembelea huko. Usishangae nikikugongea hodi siku moja.:-(

chib said...

Dar inabadirika haraka hasa kutokana na shughuli za kibiashara zinavyo ongezeka na kuwa mji ghali, lakini Kigali imezidi kwa mambo mengi.
Karibu sana Mkuu

Halil Mnzava said...

Ndio wabongo tupooo!tunasubiri tutangaziwe vivutio vyetu kwa vile ubinafsi umetuzidi.
Neno" chetu" tumeliondoa ktk kamusi,!upo hapo kaka?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hiyo ishu ya namba ukiwa unafahamu lugha za kanda ya ziwa na hasa kihaya hazikupi shida saana kwani ni mule mule tu.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hiyo ishu ya namba ukiwa unafahamu lugha za kanda ya ziwa na hasa kihaya hazikupi shida saana kwani ni mule mule tu.

chib said...

@Kamala Ndio maana mimi sikupata tabu :-)

mumyhery said...

nnahamu sana ya kufika burundi, ntajitahidi kutafuta nafasi ili niweze kutembelea burundi

chib said...

@Mumyhery: Ni muhimu utembelea sehemu roho yako inapenda. Ila Bujumbura ambao ndio mji mkubwa huko, mimi niliona na ka mji tu, sasa wewe uliye Japan, waweza kuzani umeelekea kijijini :-)

Fadhy Mtanga said...

Kaka Chib nilikuwa na mpango wa kutembelea Kigali mwisho wa mwaka huu. Lakini nadhani nitembelee Bujumbura kwanza. Wacha nifanye kazi kwa bidii nikusanye vijisenti.
Napenda sana kufahamu maisha ya watu wa Rwanda na Burundi ya sasa. Nina hamu kweli.