Member of EVRS

Friday 18 September 2009

Uganda: Nani wa kulaumiwa?


Hii sheria ya wapi! Nafikiri wale jamaa wawili wameshapata khabari kwenye makalio yao pia




Wiki iliyopita kulikuwa na vurugu Jijini Kampala ambazo zilijitokeza baada ya Kabaka Ronald Mutebi kupigwa kizuizi na Serikali ya Uganda cha kwenda kuzuru wilaya ya Kayunga kwenye sherehe ya vijana. Kwenye wilaya hii kuna mchanganyiko wa makabila mbalimbali ikiwa ni pamoja na kabila dogo la Banyala ambao hawataki kabisa uwepo wa Kabaka.
Serikali ilidai ni kwa sababu ya kiusalama, lakini kizuizi hiki kilisababisha vifo kadhaa vya wananchi waliopinga kizuizi hicho, machafuko hayo yalienda sambamba na uharibifu wa mali pamoja na wizi.
Mimi nafikiri kuna umuhimu wa kuweka ukomo wa kiongozi, nahisi Mchungaji Yoweri amekuwa anatoa maamuzi kama vile anaongoza familia yake na kusahau kuwa Uganda ni ya waganda wote. Ni wakati muafaka wa kustaafu ili abakize kasifa fulani ambako watu watakuwa wanamkumbuka.

6 comments:

Fadhy Mtanga said...

Kaka Chib picha hizi zinavuta sana hisia na kusikitisha sana. Mchungaji Yoweri ni mfano wa viongozi wengi wa Kiafrika.
Kweli Afrika inakwenda kombo.
Usichoke.

Yasinta Ngonyani said...

Inasikitisha sana, bado tu watu wanachapana viboko?

Halil Mnzava said...

Wa kulaumiwa bado ni viongozi wetu,sidhani kama wana njia ya kukwepa lawama.

Anonymous said...

Askari kuchapa viboko raia huku kashikilia mtutu, huo ni uonevu

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

amenikumbusha mabli huyu

mumyhery said...

duh hatari kupita karibu, akikushuku tu na wewe unaweza ambiwa lala chini upate viboko, naogopa!!!