Member of EVRS

Tuesday, 29 September 2009

Yaliyojiri kwenye safari hii

Safari yangu ya Dar ilikuwa na matukio mengi ya kufurahisha.
Lakini penye mengi hapakosi na machache ya kuogofya.


Siku ya jumamosi nilikuwa nimetoka na familia kuelekea nje ya jiji kuona maendeleo ya hukoo kwa wananchi. Tukiwa kwenye high way ya kwenda Bagamoyo, kwa ghafla wife akashtukia jambo........, maana aliona mwenendo usio wa kawaida kwenye chini kidogo ya dashboard...

Alipo angalia kwa makini, hakukuwa na kosa, maana alimuona kiumbe wa malaika akitambaa taratibu kuelekea palipokuwa na gear ya gari, wakati huo mie nilikuwa nimekaza macho mbele maana mwendo kasi wa barabara hii, na uwingi wa magari, inabidi uende kwa uangalifu.

Kwa sauti ya staha na ukakamavu nikasikia mvumo wa sauti ukisema, Baba nanihii, nyoka huyo. Nilipiga jicho la haraka, na kweli alikuwa mwenyewe akielekea alikokaa waifu, ikabidi nitafute upenyo ili nisimame .. lakini nikaona anakuja kwangu hivyo nikamwambie amtwange, lakini... asilani akamkosa, na jamaa akabadili uelekeo wa kuja kwangu, na kugeuza uelekeo sijui alifikiri ndio salama huko.... Nilimtolea macho huku naelekea pembeni ya barabara, maana katikati ilikuwa ni hatari kwa magari mengine.
Niliposimama, nikaamuru watu wafungue milango waishie nje, lakini nyoka alikuwa mjanja sana, maana alishakimbilia sehemu ambayo waifu alikuwa ameweka miguu yake, na mlango ulipofunguliwa tu, yeye alikuwa wa kwanza kutoka na kutokomea porini!

Tulisimama hapo kwa dk 5 kupekua gari yote, maana watoto walikuwa usingizini kiti cha nyuma. Baadaye tuliondoka kuendelea na safari huku tukitweta.

Kwa sasa tunachukua tahadhari kupaki chini ya miti na kuacha madirisha wazi, maana hawa wageni nao jua likizidi, duh, lazima wajisalimishe.

7 comments:

Faustine said...

...Nyoka ndani ya gari kaingiaje?....Maswali ni mengi kuliko majibu.....

Candy1 said...

Nilidhani nje kumbe ndani ya gari...dooh...ningezimia!!!

zedmagel said...

Hi Chib,

Very exciting explore down the big jungle. Hope you enjoy the exploration.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mnegemtoza nauli kwani alipofika mwisho wa safari alishuka!

hivi ingekuwaje kama ungemkalia?

Yasinta Ngonyani said...

Kwli ni bahati nzuri wote mpo salama. Ila jamani kwenye gari alikuwa anatafuta nini. Ahsante kwa taarifa hii nimejifunza kitu hapa leo.

wife said...

It was a nightmare! Ila tunamshukuru Mungu.
Wife

SIMON KITURURU said...

Yani hapo ni bahati tu mlikuwa nayo. Ukifikiri uwezekano wa kumkalia ulikuwepo au tu wa kupaniki na kukosa control ya gari kitu ambacho kingesababisha ajali!

Ila swali la Dr Faustine hapo juu limenifanya nikumbuke pia mdau wangu ambaye alishawekewa nyoka makusudi chumbani na sumu ya mamba kwenye maji yakuogea a.k.a ze beseni katika kuendeleza swala zima la KWANINI YEYE na SIO MIMI Kimaisha. Nimekupata lakini katika ufafanuzi wa kuwa nyoka alikimbia jua lakini.

DUH!
Poleni sana na msukosuko!