Member of EVRS

Saturday, 23 May 2009

Main Post Office - Kigali, Rwanda.


Post office letter boxes



Jana nilikwenda Posta kuu hapa jijini Kigali kuchukua "parcel" yangu niliyotumiwa kutoka ughaibuni (Nje ya Rwanda), wakati naelekea sehemu ambayo huwa wanatunza hiyo mizigo, nilipita kwenye masanduku binafsi ya barua.

Nilibaki nimeshangaa kwani ni ya mbao, na yote yana makufuli ya aina mbalimbali ambayo ndio hutumika kufunga au kufungua boksi lako kama unataka kuchukua barua, nafikiri kutokana uwezo wa mmiliki, anachagua aina ya kufuli la kuweka. Mengine kwa kweli yalikuwa makubwa kuliko kijisanduku chenyewe.

3 comments:

Fadhy Mtanga said...

Ahsante kwa picha nzuri. Pia shukrani kwa kuzuru kibarazani kwangu. Tupo pamoja.
Wikendi njema.

Mzee wa Changamoto said...

Ama kweli TEMBEA UONE. Kisha UONESHE kama hivi ulivyofanya. Asante kutujuliha yanayojiri huko "ughaibuni"
Blessings

Simon Kitururu said...

Nilipokuwa Mazengo Dodoma ndipo nilianza kuogopa kufuli.

Bwenini kwetu kulikuwa na dogo mmoja (nimemsahau jina , nakumbuka alikuwa nusu M-HUNGARY) alikuwa anauwezo wa kufungua karibu kufuli za aina zote tulizokuwa tunatumia bwenini.

Ilikuwa ukipoteza ufunguo wa kufuli yako unamwita anaiangalia halafu anaenda kutafuta nyenzo, dakika tatu hazipiti kufuli yako imefunguka.