Member of EVRS

Wednesday, 27 May 2009

Dhana ya "ung'arishaji" wa uso


Ni siku nyingi tangu nimewaona akina dada huko nyumbani Bongo waliokuwa wanapenda kubadili nyuso zao kwa "kuzing'arisha"(kuchubua) kwa kutia nakshi(Mkorogo) na kuwa na uso iliosawajika na kuwa wenye rangi "hafifu" kuliko iliyokuwapo awali, na wakati huo kuacha sehemu nyingine ya mwili kuwa asilia na iliyokolea.
Kuna baadhi ya watoto wadogo waliokuwa watukutuku nyakati hizo, walikuwa wanatulizwa kwa kuambiwa nitamuita fulani (aliyeng'arisha uso), maana kuna wengine walikuwa wanatisha baada ya zoezi la ung'arishaji.
Majuzi nilikutana na "mng'arishaji" mitaa ya huku, kwangu ilinikumbusha historia....
Wataalamu wa ngozi watanisaidia kukemea kitendo hiki, kwani mbali ya kuharibu muonekano wa mwili, pia kemikali zinazotumika katika mchanganyiko huo wa ung'arishaji zina madhara makubwa katika mwili wa binadamu na hasa zinapotumika kwa muda mrefu.
Bofya picha kwa muonekano mzuri zaidi.

16 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hakika hii ni mada nzuri nimefurahi umeiweka hapa. Kwani sijaweza kuelewa kwa nini watu wanabadili rangi walizaliwa nazo.
Unaweza kusema binadamu hatosheki na alichonacho/alichopewa. Wazungu wanataka kuwa waafrika na waafrika wanataka kuwa wazungu. Waafrika wanabadili hadi nywele zao. Kisa anataka kuwa "mzungu". Juzi nilipokuwa nyumbani TZ, nilionana na dada mmoja aliyejichubua. Na sasa sura yake inaanza "kubomoka" haribika. Amepata viupele ambavyo vimemharibu kabisa na sasa anajificha tu.

Mfano mwingine ni mwanamziki Michael Jackson. Amejiharibu kabisa. Bado sijaelewa kwa nini watu wanakimbia ASILI yao?

Thom said...

Yaonekana hata huyo dada aliyekaa chini anamshangaa mwenzake kwa kuwa na rangi mbili.
Ahsante kwa mada hii.

Anonymous said...

Urembo huu nao! Kuna ubaya gani kubakia na rangi yako ya asili?

Chama said...

Mimi nafikiri si urembo, bali ni ujinga, samahani kwa walioguswa

Fadhy Mtanga said...

Urembo, ni balaa. Ama wanapotoka na ile methali, ukitaka uzuri shurti udhurike?

chib said...

Hapo Bwana Mtanga umeniacha hoi, kwa mtindo huo, hatutafika mbali.

Ivo Serenthà said...

Hello my friends,Chib, happy to have you encountered, I am fascinated by your interesting and colorful land, Africa is always in my heart.

Good night, Marlow

jaz@octoberfarm said...

hi chib...can't understand your post! wish i knew the language! check out the new pics on my blog. you will like it! joyce

jaz@octoberfarm said...

wow chib...i just saw your post with the 2 babies...i am with you..i would not have known what to do but would have been very concerned for the babies! how awful! joyce

Simon Kitururu said...

Nasikia eti ni siye wanaume tunasababisha wajichubue kwakuwa hatuvutiwi na cheusi dawa!

Ila Congo naona ni wanaume zaidi wanajichubua a.k.a kujing'arisha!

Mzee wa Changamoto said...

Hii ni dalili ya wali kuwa mtu "kajipoteza" na anajitafuta wakati anazidi kujipoteza.
Wanatisha maana hawawezi kuwa wanavyotaka kuwa kwa muda mrefu. Umri, ukata na hata nyakati na mazingira huwafanya warejee wasikotaka na bahati mbaya huwa wanarejea na muonekano m'baya zaidi.
Asante kwa mada

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hata kama wangezaliwa weupe, bado wangatamani kuwa weusi. ni kama ufisadi, wewe unaiba hamsini, yule buku na mwingine mabilioni. ni maisha tu ya kujitafuta kwenye miili wakati sisi sio miili bali ni zaidi ya miili

jaz@octoberfarm said...

hi chib...there is a widgit you can add to your blog which translates your post. touchoutou has it on her posts. i really like seeing your blog. my husband spent a lot of time in zimbabwe and tanzania.

chib said...

Hi Joyce, I will try, however, most of them they do not have swahili translation. I will visit Touchoutou soon

Bennet said...

MI nahisi wanaojichubua sababu kubwa ni sisi wanaume, tukiamua tuachane na wanawake waliojichubua na wao wataacha kujichubua lakini kama tutaendelea kushobokea mikorogo na wao wataipaka sana, hasa huku uswahilini tulipo kina sisi ndio kama mashindano

mumyhery said...

labda nami nimuunge mkono Yasinta kwa kusema binaadam hatosheki, kwani nakumbuka kuna wakati nafanya kazi bongo kuna engineer wetu mmoja alikuja toka uk alifika jumamosi na jumapili tulimpeleka bahari beach kuogelea lakini yeye akawa anaota jua tu ili ageuke rangi alijianika siku nzima, usiku alipo lala akaanza kuumwa kumbe aliungua yaani alikuwa anashindwa kutekbea anatembea kama mwenye ukoma mikonoo anaiweka kama ndege anataka kuruka, ilikuwa afunge security camera za air port akashindwa aikabidi juma tatu tumtafutie ndege arudi nyumbani, na akaja mwingine badala yake, yaani yeye nia yake alikuwa anataka abadilike rangi matokeo yake akaungua na kazi iliyo mleta ikamshinda, isitoshe hata hapa japan kwenye african festa msheherashaji wetu nae hivyo hivyo kama unavyo muona alijianika ili ageuke rangi, hivyo nafikiri hatutosheki weusi wanataka wawe weupe na weupe wanatake wawe weusi