Member of EVRS

Friday, 15 May 2009

Kwa Taarifa Yako

Kwa utafiti uliofanywa na wanasayansi, inasemekana ya kuwa wanawake wengi (labda kwa kutokujua) hupendelea kuolewa na wanaume wenye harufu (body odour) tofauti na wao.

Utafiti huo umebaini pia kwamba utofauti huo wa harufu una kinga nzuri ya kiafya kwa watoto wanaowazaa. Lakini haijaweza kubainika ni kwa namna gani.

Swali: Watu wenye vikwapa, miguu inayopunga hewa nk. ni kweli hupata akina dada watanashati wenye harufu murua? and vice versa!!

6 comments:

SIMON KITURURU said...

Hii research inawezakufanya mtu akaacha kuoga :-)

Anonymous said...

Wanaume wote huwa wananuka miguu, wachache sana unakuta wako poa.

Anonymous said...

Usije ukajidanganya kuacha kuoga. Wanawake wengi wana artificial odour

Faustine said...

Ha ha ha! Sasa Mkuu unataka kuacha kuoga?

chib said...

Anonimy 4:25 ametoa onyo, mimi naendelea na ka-odor kangu. Ukiona mwanao hali ya afya yayumba jua - wrong choice from your wife(utafiti wadai wanawake ndio huchagua!!)

Yasinta Ngonyani said...

Kazi kwelikweli! nimepita kukusalimu nimekuona sehemu katika pitapita. karibu kibarazani kwangu