Member of EVRS

Friday 10 August 2012

Mpaka wa Tanzania na Malawi: Hali ya Wasiwasi Yatanda Malawi

Mara baada ya waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania, Bernard Membe kutangaza katizo la makampuni yanayofanya utafiti wa mafuta na gesi katika ziwa Nyasa upande wa Tanzania kupitia nchi ya Malawi kuacha kazi hiyo mara moja. Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha Taifa cha Msumbiji, kimesema wananchi wa Malawi wanaoishi karibu na Tanzania ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Malawi wa Lilongwe, wameingiwa na hofu ya kutokea vita baina ya nchi yao na Tanzania. 
  
Kwa mujibu wa Kituo cha matangazo ya runinga ya Msumbiji, kauli za Membe na mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya masuala ya usalama na mambo ya nje, Edward Lowasa, zimesababisha baadhi ya wakazi wa maeneo hayo kujiandaa kuhama maeneo yao iwapo mapigano yataanza.  
   
Waziri wa mambo ya nje wa Malawi, Ephraim Chiume, aliwatoa wasiwasi wananchi wa Malawi kwa kusema mazungumzo ya kidiplomasia na Tanzania yamekwisha anza, japo alisisitiza ya kuwa upande wa mashariki wa ziwa nyasa linalopakana na Tanzania ni mali ya Malawi kwa mujibu wa makubaliano ya wakoloni wa kiingereza na Wajerumani unaoitwa Heligoland wa mwaka 1890 ambao Malawi wanadai unatambuliwa na Umoja wa Afrika. 
  
Kwa upande wa Tanzania, hawautambui mkataba huu, ila wao wanafuata ule wa awali kabla ya makubaliano ya wakoloni hawa.
  

No comments: