Member of EVRS

Sunday, 12 August 2012

Dk. Steven Ulimboka Arejea Tanzania

Leo mchana, Dr Steven Ulimboka amerejea nchini akiwa buheri wa afya na nguvu kamili. 
 
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ghafla ulifurika watu ambao wengi wao hawakutegemea kurudi kwa Dk Ulimboka.
Katika makundi yaliyoenda kumpokea ni pamoja na jopo la madaktari wenzake na wana harakati wa haki za binadamu.

Kwa maneno machache kabisa, Dk Ulimboka amesema ya kuwa ni yeye kwa sasa ni mzima kabisa, na yupo tayari kuwajibika kwa shughuli yoyote ndani ya uwezo wake.  
   
Nao madaktari wenzake, mbali ya kufurahia ujio wake akiwa mzima, wameendelea kusisitiza ya kuwa ni muhimu kwa serikali kuweka vifaa na madawa ya kutosha kuwahudumia wananchi hapa nchini, kwani sio wananchi wote wanaweza kupelekwa nje kwa matibabu ambayo hayapatikani nchini.
 
Neno langu....... sitegemei tena kuwepo na jaribio lingine la kumteka na kumjeruhi mtu huyu. Ni muhimu sana waliolitenda tukio hili wapewe stahiki yao ili kuondoa wingu la uoga na kutokuaminiana. Nina imani jamii ya madaktari na ile ya wanatuhumiwa waliotenda tukio hili wanahitaji kufanya kazi kwa ushirikiano zaidi kuliko hali ya kutokuaminiana iliyopo sasa.

Kila la heri Dk Steven Ulimboka

No comments: