Member of EVRS

Saturday, 25 August 2012

Rais Kagame Aahidi Kuendelea Kudhamini Kombe la Kagame, Yanga nayo Yapata ushindi Kigali

Rais Paul Kagame akipokea Kombe la Kagame kutoka kwa nahodha Haroub (Kushoto) na Kocha mkuu Saintfiet (Kulia) wa Yanga ambao walifanikiwa kushinda michuano ya Kagame ya Afrika mashariki na kati kwa mwaka 2012
Siku ya Juzi, Rais Kagame wa Rwanda alilipokea kombe ambalo limepewa jina lake kutoka kwa nahodha na kocha wa timu ya mpira wa miguu ya Yanga ya Tanzania.
Mbali ya kulipoke kombe hilo, aliahidi na kupendelea udhamini wake wa kombe hili uendelee hata pale atakapo staafu na mambo ya siasa. 
   
Rais Kagame amekuwa akitoa jumla ya dola za Kimarekani 75,000 kila mwaka kwa Shirikisho la soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA). Kati ya hizo, dola 60,000 zinaenda kwa washindi wa kwanza hadi wa tatu, na dola 15,000 kuendesha shughuli za michezo hiyo. 

  
Mazoezi ya timu ya Yanga, Kigali

Timu ya Yanga ilienda Kigali, Rwanda kwa mwaliko wa rais Kagame mwenyewe, na imepangiwa kucheza michezo mitatu ya kirafiki, wa kwanza ulikuwa siku ya ijumaa tarehe 24 Agosti 2012 dhidi ya Mabingwa wa soka nchini Rwanda, Rayon sports, ambao wenyeji, yaani Rayon sports, wamefungwa magoli 2 - 0. 
   
Mbali na mwaliko huu walioupata Yanga kutoka kwa Rais wa Rwanda, pia wamepata mwaliko mwingine kutoka kwa Rais wa Tanzania.  
   
Picha na sehemu kubwa ya habari kwa kimombo nimeitoa hapa, na picha na maelezo kiasi ya Rwanda yanapatikana hapa japo yapo kwa lugha ya kinyarwanda!

No comments: