Member of EVRS

Tuesday, 28 August 2012

Bila Onyo... Mambo hayaendi!


Wakati niliokuwa natembea mitaa ya katikati ya jijini Kampala, Uganda kwenye siku za mwisho wa wiki nilikutana na bango hili. 
Nafikiri nia ni nzuri kuwatishia nyau madereva wasiojali sehemu wanapoegesha magari yao.
  
Lakini naona hilo tozo la adhabu ni dogo, kwani ni sawa na dola 2 tu za kimarekani!  
 
Kilichonkiuna zaidi.... miaka 4 iliyopita, nilipita eneo hili, lilikuwa na uzio kama huu, sasa sijui huko ndani wanajenga nini ambacho kwa miaka 4 hakijaweza kuonekana! 
  
Naendelea kuchanja mbuga!

2 comments:

emu-three said...

Wanachimba madini

Yasinta Ngonyani said...

Au wamelima kitu ambacho hawataki wengi wajue au kinazuiwa:-(