Member of EVRS

Thursday, 30 August 2012

Rwanda: Makahaba wauawa na Watu Wasiojulikana

Kumezuka wimbi la mauaji ya wasichana Nchini Rwanda. Mpaka sasa wanaohusika na mauaji hayo hawajajulikana.  
Mauaji hayo yanawalenga wasichana makahaba. Kwa mwezi huu wa Agosti pekee, wasichana 15 wamekwishauawa kwa njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na kukatwa katwa kwa vitu vya ncha kali au kunyongwa.  
Jana mchana kuna habari ya kuwa wasichana watatu waliuawa kwa kunyongwa kwenye nyumba moja ambayo ipo sehemu ya makazi ya watu wengi. Mauaji hayo yanahisiwa kufanywa nyakati za mchana.  
Hata majirani walistaajabu kupata habari za vifo hivyo, bila wao kusikia au kuhisi chochote.
Kwa sasa, katika nchi ya Rwanda, masuala ya kuendesha shughuli za ukahaba ni kosa la jinai.  
  
Hakuna shaka mauaji haya hayahusiani na vyombo vya dola, bali kuna uwezekano yanaendeshwa na watu wanaochukia shughuli za ukahaba. 

No comments: